Obama na Putin wakubaliana kuhusu Syria
Rais Barack Obama amesema yeye pamoja na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin, wamekubaliana kuhusu umuhimu wa kumaliza ghasia nchini Syria.
Bwana Obama amesema Marekani na Urusi zingependa
kuona suluhisho la kisiasa linapatikana nchini Syria na katika
kufanikisha hilo watashirikiana na pande nyingine za kimataifa kujaribu
kufikia lengo hilo.
Viongozi hao wawili wamejikuta kuwa na mwelekeo
wa pamoja katika masuala mengi kuhusu Syria wakati wa mazungumzo yao nje
ya kikao cha G20 nchini Mexico.
Viongozi hao wamejitahidi kuonyesha kuwa mkutano wao uliodumu kwa muda wa saa mbili umeimarisha uhusiano kati yao.
Rais Obama na mwenzake Putin, wamesema kuwa kuna
masuala kadhaa kuhusu juhudi za kusitisha maafa nchini syria ambayo
wamekubaliana kimsingi.
"Tumejadiliana kuhusu Syria na tumekubaliana
kuwa lazima ghasia zisitishwe na lazima tuwe na mikakati ya kisiasa
kuzuia vita vya wenyewe kwa wenyewe na maafa ambayo tumeshuhudia katika
kipindi cha hivi karibuni" alisema Rais Obama.
Uhusiano kati ya Marekani na Urusi haujakuwa mzuri sana tangu Rais Putin arudi madarakani mwezi May mwaka huu.
Rais Putin hakuhudhuria mkutano wa viongozi wa
mataifa tajiri duniani G8 uliofanyika mjini Washingnton nchini Marekani,
na wengi walihisi kuwa alisusia mkutano huo.
Rais Obama alielezea mkutano wao kuwa wa uwazi na wakina, lakini maneno aliyotatumia yamedhihirisha kuwa pia walitofautiana.
No comments:
Post a Comment