MSEMAJI WA LIL KIM AONGEA KUHUSU DISS ILIYOTANGAZWA KWA DRAKE.

.Mwakilishi wa rapper Lil Kim
amekanusha stori zilizoenea kwamba rapper huyo wa kike amemdiss Drake
kwa kitendo chake cha kuhusika kwenye ugomvi na mwimbaji Chris Brown
kwenye club moja ya usiku huko New York Marekani.
Lil Kim alidaiwa kusema Drake
amejishushia hadhi, ni mchochezi na mpuuzi tu na alichofanya kwa CB ni
kitendo cha uoga, kauli ambayo mwakilishi huyo amekanusha haikutoka kwa
lil Kim kama ilivyonukuliwa na gazeti la the Phoenix Times.
Ugomvi wa Chris Brown na Drake
uliotokea wiki iliyopita na bado umeendelea kubeba headlines duniani
kutokana na stori nyingine kadhaa kujitokeza baada ya huo ugomvi.