KINGINE KILICHOTOKEA KWENYE HII CLUB PALIPOTOKEA UGOMVI WA CHRIS BROWN NA DRAKE.
W.I.P. na Greenhouse, Club
mbili ambazo ziko kwenye jengo moja, club za usiku huko New York
Marekani palipotokea ugomvi wa kurushiana chupa kati ya mastaa wa muziki
rapper Drake na mwimbaji Chris Brown zimefungwa kwa muda.
Wengi wamejiuliza inawezekanaje
club hizo mbili zikawa zimefungwa kwa sababu hiyo tu? Kwa mujibu wa
polisi wa New York NYPD club hizo zimeripotiwa kutokea ugomvi mara
kadhaa kabla ya Chris na Drake ambao walipigana na kurushiana chupa.
Msemaji wa NYPD amesema
kufungwa kwa club hizo kumetokana na kukiukwa kwa masharti na
makubaliano kati ya wamiliki wa club hiyo na polisi wa New York ambapo
Meneja wa club hizo Jonathan Cantor pia anashikiliwa na polisi kwa
sababu ya kutoripoti kwenye kituo cha polisi mara kadhaa kama
alivyotakiwa.
Drake anadaiwa kumpiga Chris
Brown pamoja na kumchana na chupa kwenye kidevu baada ya Brown
kumuagizia pombe wakati alimuona kwenye angle moja ya club hiyo.
Chris na Drake hawapatani na
usiku huo walijikuta wote kwenye club moja, Chris alipomuona mwenzake
aliamuagiza muhudumu kumpelekea Drake pombe, Drake alikasirika na
kumfata CB na kupandishiana pamoja na kuanza kurushiana maneno kuhusu
Rihanna ambae inadaiwa wanamgombania.
No comments:
Post a Comment