Pope BenediXVI ataka amani Nigeria
Kiongozi wa kanisa Katoliki
duniani, Papa Benedict XVI ametoa wito wa kokomeshwa kwa kile
alichokitaja kama mashambulizi ya kigaidi dhidi ya wakrito nchini
Nigeria.
Papa Benedict XVI aomba utulivu Nigeria
Kiongozi huyo alikuwa akizungumza mjini Vatican wakati wa hotuba yake ya kila wiki.
Siku ya jumapili makanisa matatu yalishambuliwa na watu wa kujitolea mhanga na kusababisha vifo vya watu 16.
Wanaharakati wa Boko Haram walidai kuhusika na shambulizi hilo.
Kutokana na shambulizi hilo la jumapili
,kumekuwa na mashambulizi mwengine ya ulipizaji kisasi katika miji ya
Kaduna na Damaturu na kusababisha vifo zaidi.
Lakini katika hutuba yake Papa Benedict amewataka wa-Nigeria wajenge jamii iliyona maelewano.
Amsema amekuwa akifuatilia kwa masikitiko
makubwa yale yanayotokea nchini Nigeria ambapo mashambulizi ya kigaidi
yanaendelea hasa yakielekezwa kwa wa-kristo.
Papa ametaka hali hiyikomeshwe ili kuzuia umwagikaji zaidi wa damu nchini humo.

No comments:
Post a Comment