Mtangazaji wa Kituo cha Runinga cha Star, Rachel Ndauka jana aliangusha bonge la pati ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ‘bethidei’ ambayo ilitawaliwa na shangwe za hapa na pale sambamba na vituko vya kila aina. Sherehe hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Hazina Lounge uliopo katika Ufukwe wa Coco jijini Dar ambapo Rachel alitimiza miaka 22 na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki na filamu huku suala la burudani likishika kasi mwanzo mwisho.
No comments:
Post a Comment