BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Tuesday, April 16, 2013

MAKUBWA HAYA!...

INAUMA sana! Mwanamke ambaye alibaki na vipande vya mabomu mwilini yaliyompata kutokana na mlipuko wa mabomu Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, Jenifa Msigwa (27), amefariki dunia na maiti yake kusababisha igombewe. Jenifa alikuwa mjasiriamali maeneo ya Gongo la Mboto ambapo mabomu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) yalipolipuka akiwa kwenye shughuli zake, vipande vya vyuma vilimuingia mwilini na kubaki navyo hadi alipofariki dunia Aprili 8 mwaka huu ambapo maofisa wa jeshi walizuia kuchukuliwa kwa maiti.

Habari zinasema wanajeshi walikasirika baada ya kuona ndugu hawakuwashirikisha katika hatua za mwisho, hasa baada ya Jenifa kuzidiwa wakati walikuwa wakimhudumia wakati wa ugonjwa wake. “Wanajeshi walishukizwa kutokana na ndugu wa marehemu kumpeleka hospitali mgonjwa bila wao kupewa taarifa kwani alikuwa na vyuma mwilini,” kilisema chanzo. Vyuma hivyo vilimsababishia ulemavu wa kupooza kuanzia kiunoni mpaka miguuni na hakuweza kusimama tena mpaka alipofariki dunia wiki iliyopita. Akizungumza kwa huzuni huku akilengwalengwa na machozi baba mzazi wa marehemu, Mzee Msigwa alisema, “ Aprili 8, mwaka huu mwanangu Jenifa alizidiwa ghafla akiwa nyumbani kwangu Urafiki, Dar kwani alikuwa akitapika sana kutokana na kibofu cha mkojo kuziba ambapo tulifanya jitihada za kumkimbiza hospitali lakini alifariki akiwa njiani. “Chanzo cha tatizo hili ni mabomu yaliyolipuka Gongo la Mboto mwaka juzi, aliathirika kwani alijeruhiwa na akawa anatibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa ambapo alikuwa akihudhuria kliniki kila mwezi. “Baada ya uchunguzi wa madaktari waligundua kuwa ana vipande vya vyuma mwilini na wakabainisha kuwa haviwezi kuondolewa,” alisema Msigwa. Hata hivyo, alisema serikali ilitoa ushirikiano wa kutosha kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa kwani kila mara walikuwa karibu sana na mgonjwa huku wakimpa huduma mbalimbali zinazostahili kupewa mgonjwa mpaka mazishi yake yaligharamiwa na serikali. “Naishukuru serikali kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa kwa ushirikiano walioonesha kwa mwanangu kuanzia matibabu hadi mazishi yake sina cha kuwalipa ila naamini wataongezewa zaidi kwani mimi peke yangu nisingeweza,”alisema mzee huyo. Aliongeza kuwa pengo la kuondokewa na mwanaye halizibiki kwani alikuwa ndiye mlezi wa wadogo zake kwa sababu mama yao alishafariki hivyo alikuwa akiwasomesha na kuwasaidia mahitaji mengine muhimu. Aprili 10 mwaka huu mwili wa marehemu Jenifa uliagwa nyumbani kwao Urafiki na baadaye kuzikwa katika makaburi ya Mburahati jijini Dar es Salaam.

JWTZ, FAMILIA WAGOMBEA MWILI INAUMA sana! Mwanamke ambaye alibaki na vipande vya mabomu mwilini yaliyompata kutokana na

mlipuko wa mabomu Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, Jenifa Msigwa (27), amefariki dunia

na maiti yake kusababisha igombewe. Jenifa alikuwa mjasiriamali maeneo ya Gongo la Mboto ambapo mabomu ya Jeshi la Wananchi wa

Tanzania (JWTZ) yalipolipuka akiwa kwenye shughuli zake, vipande vya vyuma vilimuingia

mwilini na kubaki navyo hadi alipofariki dunia Aprili 8 mwaka huu ambapo maofisa wa jeshi

walizuia kuchukuliwa kwa maiti. Habari zinasema wanajeshi walikasirika baada ya kuona ndugu hawakuwashirikisha katika hatua

za mwisho, hasa baada ya Jenifa kuzidiwa wakati walikuwa wakimhudumia wakati wa ugonjwa

wake. “Wanajeshi walishukizwa kutokana na ndugu wa marehemu kumpeleka hospitali mgonjwa bila wao

kupewa taarifa kwani alikuwa na vyuma mwilini,” kilisema chanzo. Vyuma hivyo vilimsababishia ulemavu wa kupooza kuanzia kiunoni mpaka miguuni na hakuweza

kusimama tena mpaka alipofariki dunia wiki iliyopita. Akizungumza kwa huzuni huku akilengwalengwa na machozi baba mzazi wa marehemu, Mzee Msigwa

alisema, “ Aprili 8, mwaka huu mwanangu Jenifa alizidiwa ghafla akiwa nyumbani kwangu

Urafiki, Dar kwani alikuwa akitapika sana kutokana na kibofu cha mkojo kuziba ambapo

tulifanya jitihada za kumkimbiza hospitali lakini alifariki akiwa njiani. “Chanzo cha tatizo hili ni mabomu yaliyolipuka Gongo la Mboto mwaka juzi, aliathirika kwani

alijeruhiwa na akawa anatibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa

ambapo alikuwa akihudhuria kliniki kila mwezi. “Baada ya uchunguzi wa madaktari waligundua kuwa ana vipande vya vyuma mwilini na

wakabainisha kuwa haviwezi kuondolewa,” alisema Msigwa. Hata hivyo, alisema serikali ilitoa ushirikiano wa kutosha kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa

kwani kila mara walikuwa karibu sana na mgonjwa huku wakimpa huduma mbalimbali

zinazostahili kupewa mgonjwa mpaka mazishi yake yaligharamiwa na serikali. “Naishukuru serikali kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa kwa ushirikiano walioonesha kwa mwanangu

kuanzia matibabu hadi mazishi yake sina cha kuwalipa ila naamini wataongezewa zaidi kwani

mimi peke yangu nisingeweza,”alisema mzee huyo. Aliongeza kuwa pengo la kuondokewa na mwanaye halizibiki kwani alikuwa ndiye mlezi wa

wadogo zake kwa sababu mama yao alishafariki hivyo alikuwa akiwasomesha na kuwasaidia

mahitaji mengine muhimu. Aprili 10 mwaka huu mwili wa marehemu Jenifa uliagwa nyumbani kwao Urafiki na baadaye

kuzikwa katika makaburi ya Mburahati jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...