IMEBAINIKA kwamba kuna mtandao wa askari ndani ya majeshi mbalimbali ya ulinzi nchini na hasa Jeshi la Magereza ambao unajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa akionyesha baadhi ya madawa ambayo yaliwahi kukamatwa na kikosi chake.
Uchunguzi wa Uwazi umebaini kwamba tayari orodha ya majina ya askari hao yamekabidhiwa kwa Kamishna Jenerali Mkuu wa Magereza, John Minja ili kuwashughulikia kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa chanzo makini kilichopo ndani ya jeshi hilo, kilisema kwamba tayari mkakati maalum umeandaliwa ili kuwachukulia hatua askari wanaojihusisha na mtandao huo na kuahidi kwamba hakuna mtu hata mmoja atakayepona. “Taa nyekundu imewaka kwani baada ya kamishna kupata orodha hiyo aliweza kuwapangua askari wakubwa katika Gereza la Keko jijini Dar na kuwatawanya sehemu mbalimbali ili kuhakikisha kwamba mtandao huo unakoma na biashara hiyo inafikia tamati. “Pia, makachero makini wamewekwa katika kila gereza hapa nchini ili kupambana na hali hiyo na majeshi yote yatachunguzwa,” kimesema chanzo hicho.
Madawa ya kulevya.
Mkakati huo uliandaliwa kabla ya Aprili 7, mwaka huu ambapo saa 4 usiku makachero walimnasa askari magereza, Brighton Octavian, akiingia kazini katika Gereza la Keko akiwa na kete 732 za Heroin kwa madai ya kuzipeleka kwa wafungwa. Imedaiwa kuwa askari huyo ni mmoja tu kati ya watu wanaodaiwa kuunda mtandao huo ambao pia unawashirikisha baadhi ya raia na vigogo wa madawa ya kulevya hapa nchini. “Kamishna Minja amethubutu kuchukua hatua ili kurekebisha tabia na mwenendo wa magereza yetu kwa kuwa huko nyuma hali ilikuwa mbaya na kuonekana kama sehemu ya genge la kupitisha madawa ya kulevya kwa ajili ya wafungwa,” kilisema chanzo hicho. Uwazi limebaini kwamba baadhi ya askari katika magereza mbalimbali nchini wamekuwa na maisha mazuri kuliko makamishna wa magereza, hali ambayo inawashangaza wengi.
Rais Dk. Jakaya Kikwete.
Inadawa kwamba askari hao wamekuwa si waaminifu kutokana na kushiriki kwao katika mtandao huo wa biashara haramu. Baada ya Kamishna Minja kuteuliwa kuongoza jeshi hilo, aliunda tume ya kuchunguza changamoto mbalimbali na kugundua udhaifu mkubwa katika Gereza la Keko. Gazeti hili lilimsaka Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa na kumuuliza hatua wanazozichukua kutokana na hali hiyo. Mbali na kumtaja askari magereza Brighton, pia Nzowa aliongeza kuwa wapo katika mpango maalum wa kumaliza tatizo hilo ndani ya magereza nchini.
Waziri ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
“Askari aliyekamatwa alikutwa na kete 732, tunajipanga kuumaliza mtandao wao kwa nguvu zote,” alisema Nzowa na kuongeza kuwa inashangaza kuona askari nao wameingia kwenye biashara hiyo haramu. Alipoulizwa kuhusu majeshi mengine, Nzowa alisema wakuu wake ambao ni wa majeshi yote hawataki kabisa kuona biashara hiyo haramu inafanyika popote pale, hivyo yupo nao bega kwa bega kupambana na askari atakayethubutu kuifanya. Naye Msemaji wa Jeshi la Magereza, Mtiga Omari alisema askari Brighton ameshafukuzwa kazi.
“Tumemkabidhi kwa polisi ili ashughulikiwe kisheria na kuhusu majina ya baadhi ya askari wengine wa magereza wanaojihusisha na biashara hiyo naomba unipe muda nifuatilie,” alisema Kamanda Mtiga. Jeshi la polisi linaongozwa na IGP Said Mwema na kanda maalum inaongozwa na DCP Suleiman Kova ambao wote wapo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani inayoongozwa na Dk Emmanuel Nchimbi ambaye kasi yake ya utendaji kazi tangu ateuliwe kushika wadhifa huo na Rais Jakaya Kikwete, inasifiwa na wengi.
I'm really impressed along with your writing skills as neatly as with the structure in your blog. Is that this a paid subject or did you customize it your self? Either way stay up the excellent high quality writing, it is rare to see a great weblog like this one these days..
ReplyDeleteAlso visit my web site: Its About Time Grindstone Mattseh