SIKU chache baada ya Mtanzania aliyefia nchini China, marehemu Josephat Mkumbukwa Dumwe (39) kuzikwa Aprili 3, mwaka huu, inadaiwa kuwa mchongo wa kuuawa kwake aliujua mapema.
Watu wakipita kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Josephat Mkumbukwa. Kushoto ni mjomba wa marehemu Erasto Kombe.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, mjomba wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Erasto Kombe alisema marehemu kabla ya kusafiri kwenda China aligusia kwamba kuna watu wamedhamiria kumuua lakini amekufa na siri moyoni kwani hakuwataja wahusika.
Marehemu Joseph Mkumbukwa enzi za uhai wake.
“Kabla marehemu hajasafiri kwenda China zilivuja habari kuhusu kuuawa kwake lakini alipuuza kwa sababu aliamini hakuwa na adui yeyote. Bahati mbaya amefariki dunia na hakuwahi kutueleza mpango huo ulisukwa na nani na kwa sababu zipi,” alisema Kombe.
Baba wa marehemu, mzee Juma bakari, akifarijiwa na ndugu yake katika makaburi ya Buzuruga Nyakato wakati wa mazishi ya mwanaye, Mkumbukwa.
Naye baba mzazi wa marehemu, Juma Bakari Dumwe, alisema: “Siku moja kabla ya kusafiri nilizungumza na mwanangu kwa simu, akanieleza kuhusu safari hiyo, aliniahidi akirudi atanijengea nyumba nzuri. Lakini ndiyo hakurudi tena.” Mkumbukwa alifariki nchini China na maiti yake ilikaa mwaka mmoja kabla ya kusafirishwa hadi Tanzania huku kifo chake kikiacha maswali mengi.
No comments:
Post a Comment