“HUJAFA hujaumbika, Mungu ana makusudi yake na yeye ni muweza wa
yote kwani ndiye aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana
na visivyoonekana.” Hiyo ni kauli ya mzazi wa mtoto Zawadi Godfrey
Mwingune aliyezaliwa akiwa na macho matatu na kichwa mfano wa uyoga.
Akizungumza na gazeti hili wiki iliyopita mama mzazi wa mtoto Zawadi, Marthar Kitago (28) mzaliwa wa Kijiji cha Kidegembye Lupembe wilayani Njombe mkoani Njombe alisema kuwa hadi sasa anamwachia Mungu ambaye ndiye amempa zawadi ya mtoto huyo.
“Jumapili Januari 13, mwaka huu nilishikwa na uchungu nikakimbizwa katika Kituo cha Afya cha Kidegembye ambako sikukaa nikahamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Njombe Kibena ambako nilifanyiwa upasuaji na kubahatika kumpata mtoto huyu.
“Niliogopa sana baada ya kuonyeshwa mtoto wangu
jinsi alivyo ila nilipiga moyo konde kwa kuwa ni damu yangu, tukampa jina la Zawadi, tukiwa na maana ni kutoka kwa Mungu,” alisema mama huyo wa watoto watatu.
Baba wa mtoto huyo, Godfrey Mwingune anayeendesha maisha yake kwa kilimo alisema kuwa hali ya afya ya mtoto huyo si nzuri kwani mbali ya kuzaliwa na kilo 4 na nusu, bado ana tatizo la uvimbe katika paji lake la uso unaofanana na umbo la uyoga pia kichwani kuna kovu kubwa kama ncha mbili hivi ambalo linatoa usaha mwingi.
Akaongeza kuwa katika jicho lake la kushoto kwa juu kuna jicho la pili na kufanya mtoto huyo kuwa na macho matatu ambapo madaktari wamemshauri ampeleke katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Amesema fedha zinazotakiwa ili mwanaye apatiwe tiba ni shilingi 1,500,000 na amewashukuru wakazi wa Isimani ambao wamemchangia shilingi 300,000 kwani yeye hana uwezo.
Walioguswa na habari hii wanaweza kumchangia mtoto huyu kupitia namba 0754 026 299 au
0712 750 199- Mhariri.

No comments:
Post a Comment