Zambia 1-0 Uganda
Zambia
ilijipatia ushindi mwembamba dhidi ya Uganda wa goli moja kwa sifuri
lililofungwa na mshambuliaji Christopher Katongo katika kipindi cha
kwanza.
Goli hilo la upande wa Zambia lilikuja katika dakika ya 20 kwa ushirikiano mzuri wa Davies Nkausu.
Uganda hawakuonyesha makali na huenda
wakajisikia unafuu baada ya kuondoka uwanjani wakiwa wamebebeshwa goli
moja tu na Wazambia.
Uganda hawajawahi kupoteza mechi wakiwa nyumbani toka mwaka 2004, ingawaje safari bado inaendelea.
Pia katika mechi nyingine ilikuwa kama ifuatayo.
Jamhuri ya Kati(CAR) 1-0 Burkina Faso
Burkina Faso itabidi wachechemee katika raundi
yao ya mwisho ya kufuzu kuingia mashindano ya Kombe la Afrika 2013 baada
ya kufungwa goli moja na Jamhuri ya Afrika ya Kati(CAR) mjini Bangui
siku ya Jumamosi.
Watajaribu kuthibitisha uwezo wao katika hatua nyingine mjini Ouagadougou mwezi ujao.
Kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati waliowaacha mdomo
wazi mabingwa wa zamani wa Afrika Misri katika raundi za awali, matokeo
haya yanawaweka katika nafasi nzuri kufuzu fainali za Kombe la Mataifa
ya Afrika kwa mara ya kwanza kabisa.
Gabon 1-1 Togo
Goli la kusawazisha kutoka kwa Emmanuel Adebayor
aliyerejea timu ya Togo inaipa Togo nafasi nzuri katika mashindano haya
baada ya kizaazaa cha mjini Libreville.
Ilikuwa ni Gabon walioleta muafaka baada ya
mshambuliaji mkongwe Daniel Cousin kuipatia timu yake matumaini katika
dakika 15 zilizokuwa zimesalia.
Lakini Adebayor, aliyerejea baada ya kutowekea
mafichoni, alijibu mapigo na kuiweka Togo kuchungulia nafasi nyingine
mjini Lome mwezi ujao.
Ghana 2-0 Malawi
Ghana imeiadhibu Malawi magoli mawili kwa bila ikiiacha Malawi kuwa na kibarua kigumu katika mapambano ya mbele.
Christian Atsu aliipatia Ghana mwanzo mzuri hususani katika dakika nane za kwanza.
Malawi ilijikuta ikijilazimisha kuzuia machozi
baada ya James Sangala kutolewa nje wakati wa mchezo huo, na sasa
wanakibarua kigumu kujibu iwapo wataingia fainali za mashindano haya ya
Kombe la Afrika kwa mara ya tatu tu katika historia yao.
Sierra Leone 2-2 Tunisia
Siera Leone na Tunisia zimetoka sare ya mabao
mawili kwa mawili huku matumaini ya Siera Leone kuingia fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza kabisa tangu mwaka 1996 yakiwa
mashakani.
Alhassan Kamara aliongoza kwa kile alichodhania
lingekuwa goli la ushindi dhidi ya Tunisia huku zikiwa zimesalia dakika
tano tu mchezo kumalizika, lakini Youssef M'sakni akazawazisha katika
dakika mbili baadaye.
Ivory Coast 4-2 Senegal
Ivory Coast waliibuka kidedea baada ya kuichapa Senegal magoli manne kwa mawili.
Dame N'Doye alianza kwa kuingiza goli la kwanza kwa Senegal, kabla ya Salomon Kalou kujibu mapigo.
Papiss Cisse aliipatia Senegal tabasamu baada
kuongeza goli la pili kabla ya Ivory Coast kujibu mashambulizi kwa
magoli kutoka kwa Gervinho, Didier Drogba na Max Gradel.
Goli jingine kutoka kwa Drogba lilikataliwa baada ya kuushika mpira kwa mkono.
Cape Verde 2-0 Cameroon
Cameroon ilijikuta ikiaibishwa hadharani baada
ya kuchomekwa magoli mawili na Cape Verde, ikiwa ni matokeo mazuri
kabisa kuwahi kupata kwa timu ya Cape Verde dhidi ya mabingwa hao wa
mara nne barani Afrika.
Goli kutoka kwa Ricardo na pia Djaniny yamewapa
matumaini Cape Verde kuingia katika fainali za mashindano haya kwa mara
ya kwanza kabisa katika historia yao.
Kukosekana kwa Samuel Eto'o, kunaonekana kuipa
Cameroon wakati mgumu sana kupata magoli, na ukweli ni kwamba wanahitaji
magoli ili kuweza kuepuka fedheha za kutimuliwa kutoka katika
mashindano hayo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980.
Mali 3-0 Botswana
Licha ya mgogoro wa kisiasa nchini mwao Mali
waliweza kuichapa Botswana magoli matatu kwa sifuri siku ya Jumamosi,
ikijiweka katika nafasi nzuri kuelekea Afrika Kusini mwaka ujao.
Cheick Diabate anayeishi Ufaransa aliiwezesha
timu yake ya nyumbani kuongoza katika dakika 27 za mchezo wakati wa goli
la penalti, ambapo Mahamadou Ndiaye aliongeza la pili baadaye katika
dakika ya sitini.
Naye Modibo Maiga hakuwa na huruma dhidi ya
Botswana baada ya kushindilia goli la tatu lililoiacha Botswana
ikitafuta mahali pa kujificha.
Ushindi huu wa magoli matatu unaipa Mali ujasiri
wa kusonga mbele katika hatua ijayo mjini Gaberone pasipo kuwa na
wasiwasi mkubwa sana.
Sudan 5-3 Ethiopia
Ilikuwa ni siku ya kuonyeshana ubabe wa nani
zaidi katika kufungana magoli, wakati Sudan ilipoifunga Ethiopia magoli
matano huku Ethiopia ikijibu kwa magoli matatu.
Ilichukua muda wa dakika saba tu kwa goli la kwanza kuchomekwa kutoka kwake Mudather El Tayeb Karika.
Hii ilileta hasira ya kuonyeshana nani ni mbabe zaidi katika mechi hiyo.
Katika ndani ya dakika mbili Momhmad Bisha aliipatia Sudan goli na Musab Umar kuimarsha zaidi katika dakika ya 36.
Baada ya mapumziko Ethiopia ilianza kuishambulia
Sudan kwa magoli kutoka kwa Kebede na Tesfaye Alebachew yaliyoziweka
timu hizo mbili katika usawa wa magoli matatu kwa matatu kabla ya
mashambulizi mengine mawili kutoka kwake Muhannad El Tahir wa Sudan
yaliyoiacha Ethiopia ikinyoosha mikono juu kukubali mvua hiyo ya magoli
matano.
Liberia 2-2 Nigeria
Liberia ilitoka sare na Nigeria ya mabao mawili kwa mawili katika uwanja wa Samuel Doe Stadium mjini Monrovia
Omega Roberts aliipatia timu yake ya Liberia goli la kwanza katika dakika ya nane.
Lakini Nosa Igiebor alisawazisha kwa upande wa Nigeria dakika sita baadaye.
Ike Uche alifanikisha goli la pili kwa Nigeria
kupitia penalti, wakati Vincent Enyeama alipoipatia pia timu yake goli
la pili katika kipindi cha pili.
No comments:
Post a Comment