Wachimba migodi nchini Afrika Kusini wameanza kurejea kazini katika mgodi wa madini ya Platinum wa Marikana
Mgodi huo ulikuwa kitovu cha ghasia na mauaji ya
wachimba migodi 44 waliozua ghasia wakati wakigoma kwa wiki sita kudai
nyongeza ya mishahara .
Mapema wiki hii wachimba migodi waliafikia makubaliano ya asilimia 22 ya nyongeza ya mishahara ndipo wakakubali kurejea kazini.
Wamiliki wa mgodi wa Lonmin ambao ni wa tatu kwa
ukubwa katika kuzalisha madini ya Platinum duniani, walielezea kupata
hasara kubwa ya kifedha wakati mgodi huo ulipofungwa kufuatia mgomo wa
wachimba migodi.
Jopo maalum limeundwa nchini humo kuchunguza vifo vya wachimba migodi waliouawa na polisi wakati wa migomo hiyo
No comments:
Post a Comment