Kamanda wa polisi Iringa
Michael Kamuhanda amethibitisha kwamba askari polisi ambae anatuhumiwa
kuhusika na mauaji ya kukusudia ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi
amefikishwa mahakamani Iringa september 12 2012.
Askari mwenyewe ni mwenye namba G2573 na jina lake ni Pasificus Cleophace Simoni mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa FFU Iringa.
Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi
wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa
hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza
kesi za mauaji.
Kwenye kesi za jinai sheria
kifungu cha 196 iliyofanyiwa marejeo 2002 inakatazwa mtuhumiwa wa mauaji
ya kukusudia kupewa dhamana ambapo mtuhumiwa amerudishwa mahabusu
kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa
hadi 26 Septemba mwaka huu itakapotajwa tena.
Kamanda Michael Kamuhanda
amesema “ni kosa kama makosa mengine huwa yanatokea katika kazi,
uchunguzi umekamilika na mtuhumiwa amefikishwa Mahakamani”
No comments:
Post a Comment