MSANII aliyewahi kutamba na Kundi la Sanaa la Kaole la jijini Dar es Salaam ambaye kwa sasa amejikita kwenye filamu, Mwasiti Mohamed ‘Sishi’ amenaswa katika baa moja iliyopo Sinza–Mori, Dar mchana kweupe akigida konya au ‘ngumu kumeza’ huku akiwa amevalia vazi la Kiislamu ‘nikabu’.
Septemba 20, 2012, paparazi wetu alitonywa kuwa, msanii huyo
alitinga kwenye baa hiyo akiwa amevalia nikabu iliyomfunika sehemu kubwa
ya juu ya mwili wake na kubakisha uso na alipoketi aliagiza kinywaji
hicho na kuwafanya watu kumkodolea macho.
Baadhi ya watu waliokuwa kwenye baa hiyo walipata wakati mgumu kwa
kuogopa, wengine wakiamini msanii huyo ni askari ambaye alifika pale
kuwakamata watu wanaokunywa muda wa kazi hivyo wengi walikosa amani na
kuondoka.
Mwandishi wetu alipomkabili na kumuuliza kulikoni kupiga pombe kali
muda ule, alijitetea kuwa eti hakuwa akigida kinywaji hicho, ila alikuwa
kwenye baa hiyo akimsubiri mtu kwa ajili ya kufanya makubaliano ya
kucheza filamu.
“Mimi sikuwa nakunywa pombe pale, ni maji tu. Nilikuwa namsuburi mtu,
aliniambia atakuja, tunataka kuzungumza mambo ya kucheza filamu,”
alisema Sishi.
No comments:
Post a Comment