Serikali ya Mali imekubali kuwa
mwenyeji wa jeshi la pamoja la nchi za kanda ya Afrika Magharibi ambalo
litasiadia katika juhudi za kupambana na wapiganaji wa kiisilamu ambao
wanadhibiti eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo.
Nchi hiyo itatafuta uungwaji mkono wa umoja wa
mataifa baadaye wiki hii kwa ushirikiano na muungano wa nchi za
magharibi (Ecowas.)
Wanamgambo wa kiisilamu walitwaa eneo hilo mwezi Aprili na kusababisha hofu ya kuwepo vurugu katika kanda hiyo.
Awali Mali ilipinga kuwa mwenyeji wa kikosi hicho cha wanajeshi 3,000 mjini Bamako ingawa sasa imebadili msimamo wake.
Baada ya juhuzi kubwa za kidiplomasia
zikijumuisha viongozi wa kanda hiyo, maafisa wakuu sasa wametoa idhini
ya kuweza kuwa na kambi za jeshi hilo katika vitongoji vya mji mkuu.
Rais wa muda wa Mali, Dioncounda Traore alisemekana kutoridhia wanajeshi hao wageni kuwa nchini humo.
Wapiganaji hao wa kiisilamu walichukua udhibiti
wa eneo la Kaskazini mwa nchi, baada ya nchi hiyo kukumbwa na vurugu
kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwezi Machi mapema mwaka
huu.
Wapiganaji hao wameanza kutumia sheria za
kiisilamu katika miji ya Timbuktu, Kidal na Gao huku madhabahu ya kale
ambayo yanaonekana kama ambayo yanatumiwa kwa ushirikina yakiharibiwa.
No comments:
Post a Comment