Jukwaa la Wahariri Tanzania
pamoja na waandishi wa habari waliungana na kufanya maandamano kuanzia
mkao makuu ya kituo cha Television cha Channel Ten mpaka kwenye viwanja
vya Jangwani Dar es salaam september 11 kupinga mauaji ya mwandishi wa
habari Daudi Mwangosi alieuwawa kwa kulipukiwa na bomu akiwa mikononi
mwa polisi Iringa wakati polisi walipokua wakiwatawanya wafuasi wa Chama
cha Demokrasia na maendeleo.
Mjumbe wa jukwaa la wahariri
kutoka Zanzibar Masoud Sanani kwenye maandamano hayo Jangwani
alitangaza maazimio yaliyofikiwa na washiriki wa maandamano hayo,
namkariri akisema “kwa siku 40 hizi za maombolezo tusiandike habari ya
polisi, polisi hata akifanya kitu gani tusiandike, wataandika kwenye
gazeti lao la polisi wanalo”
Katibu wa jukwaa la wahariri
Tanzania Neville Meena alizungumza pia na kuamplfy kwamba vyombo vya
habari vinafanya kazi kubwa kwa kufuata taaluma na havipo kwa ajili ya
maslahi ya mtu yoyote.
Namkariri akisema “sheria zetu
ni kandamizi sana ndio maana leo hii tunahangaika, Wakuu wa Polisi
Iringa na wenzie waliohusika na lile jambo ambao ushahidi uonyesha
kabisa kwamba kuna kuhusika kwa polisi wamekaa kimya mpaka leo,
hatujasikia polisi wanasema jambo lolote mpaka leo, kwa sababu sheria
zetu zimekaa vibaya kwa hiyo jitihada za kuhakikisha tunapata sheria
mpya za habari tuendelee nazo tupate sheria mpya ili mwisho wa siku
tuhakikishe tunakua na maisha salama”
Kwenye line nyingine ni kwamba
waandishi hao wa habari walioandamana walilazimika kupinga ujio wa
Waziri wa mambo ya ndani Dr Emmanuel Nchimbi aliehudhuria maandamano
hayo Jangwani ambapo waandishi walisikika wakisema “maandamano haya ni
ya waandishi na wahariri wetu kwa hiyo Nchimbi aondoke”
Baada ya hapo sauti kupitia
kipaza sauti ilisikika ikisema “kwa sababu mmesema, tukampelekea ujumbe
Mh Waziri hawa jamaa wanasema tupishe, tunakuomba gari yako iko pale
taratibu tunaomba uondoke, amewaona akaamua aondoke… hatuna ugomvi na
serikali wala hatuna ugomvi na wizara yoyote ile ila shughuli ya leo
imemkataa na tunaomba salamu zetu zimfikie kwamba tunampenda sana, ni
rafiki yetu ni waziri wetu lakini hakuwa na vazi la msiba”
No comments:
Post a Comment