Hii post inamuhusu aliekua mbunge wa Arusha mjini kupitia CHADEMA Godbless Lema ambae alivuliwa ubunge na Mahakama.
Kuna mambo mengi niliyotamani
kumuuliza kabla ya kukutana nae ambayo hata hivyo nilimuuliza na yote
akayatolea ufafanuzi kwenye hii exclusive interview.
Kuhusu kupata vitisho, Lema
amesema “kutishwa, kutukanwa ama watu kukufatilia wengine kukutishia
wengine kujifanya wanakuangalia kimpango, taarifa hizo ni nyingi lakini
hivyo sio vitu vya kunitisha wala sitembei na mlinzi na siogopi
nitaendelea kufanya kazi ya ukombozi kwa sababu kwanza siwezi kuishi
milele, kuna watu hawafanyi harakati za ukombozi lakini wako wanakufa
Muhimbili kwa magonjwa kama Malaria”
Kwenye sentensi ya nyongeza
naendelea kumkariri Lema akisema “mimi ni bora nikapigwe risasi lakini
mchungaji akija kusoma risala aseme marehemu amekufa akipigania haki,
kifo kwangu kimeshapoteza kumbukumbu na uoga kwangu umeshapoteza
kumbukumbu, siogopi kufa siogopi jela ila naogopa kwenda jela kwa wizi
wa kompyuta, Tv au kubaka mwanamke lakini siogopi kwenda jela kwa
kupigania haki za watu, wanaoleta vitisho ninawakaribisha.. ni vingi na
vingine tunavifanyia utafiti sisi wenyewe tujue chanzo ni nini, hata
muundo wa serikali ulivyo dhidi ya wapinzani ni kitisho namba moja,
kwamba wewe ni mbunge wa Chadema na unafanya kazi na DC ama na mkuu wa
mkoa ambae ni mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM wilaya”
Kauli nyingine aliyoitoa Lema
ni kuhusu kesi yake kwa sasa kwa kusema “sitaki mahakama ya rufaa
inipendelee sitaki hata kidogo, ikinipendelea nitalia, nitaogopa
nitasikitika nikijua nilifanya makosa ya kuua alafu nikaachiwa huru,
niko tayari kurudi kwenye uchaguzi na nitashinda kuliko mbunge yeyote
Afrika Mashariki kwa kura za kubeba na Canter ila ninachotaka ni haki
itendeke, ila nimepata faraja kwamba anaeiongoza kesi yangu ni jaji mkuu
wa Tanzania nikiamini atapitia vipengele vya kisheria vizuri kabisa”
Pamoja na hayo yote, Godbless
Lema amesema hajawahi kujuta kuwa nje ya bunge ila anajuta kwa nini
Mahakama iliingiliwa na kumfanya ajue matokeo ya kesi siku 14 kabla
ambapo namkariri akisema “Halima Mdee alinipa matokeo ya kesi mpaka
kifungu kinachokwenda kunibana, Dr Slaa anaingia mahakamani ananiamba
mwanangu unakwenda mahakamani lakini hukumu yako itakua hivi, ile kesi
hukumu ilivuja kwa hiyo maana yake ilikua ni mpango, ni kitu kimepangwa”
“Kilichoniumiza sio mimi
kutokua mbunge, ninaweza kuishi nje ya Ubunge ninaweza kuuza mitumba,
ninaweza kuwa dereva wa daladala, ninaweza kucheza soka.. ubunge kwangu
sio ajira naweza kuishi maisha mazuri kuliko kuwa mbunge, nimekua
mfanyabiashara siku za nyuma sijakwenda Ulaya nikiwa mbunge, nimekwenda
ulaya kabla sijawa mbunge nimekwenda karibu nchi 16 na nimefanya
biashara lakini nilipopata ubunge nikasema nimepata nafasi ya kutumikia
watu”
Godbless Lema, licha ya kuhusishwa na mtandao wa magari, ni mvuta bangi, mdini na tapeli.
ReplyDelete