Mabingwa watetezi wa klabu
bingwa barani Ulaya, Chelsea ya Uingereza, wakicheza katika uwanja wa
nyumbani wa Stamford Bridge, walishindwa kuifunga Juventus ya Italia
katika pambano la Jumatano usiku.
Nyota wa Chelsea alikuwa ni mchezaji Oscar
kutoka Brazil, ambaye alifanikiwa kutumbukiza magoli mawili wavuni
katika kipindi cha kwanza; dakika ya 31 na 33.
Bao la pili liliingia kupitia mkwaju wa mbali, na ambalo lilimuacha kipa wa Juventus, Gianluigi Buffon akiwa amezubaa.
Oscar alisajiliwa na Chelsea hivi majuzi.
Oscar alisajiliwa na Chelsea hivi majuzi.
Hata hivyo Juventus, mabingwa wa Italia, na
ambao hawakushindwa katika mechi 42 za Serie A huko nyumbani,
walijikakamua na hatimaye kusawazisha na kujinyakulia pointi moja.
Arturo Vidal aliwafungia bao kabla ya kipindi
cha kwanza kumalizika, na baadaye mchezaji wa zamu, Fabio Quagliarella,
zikiwa zimesalia dakika tisa mechi kumalizika, alithibitisha Juventus
ilikuwa na nia ya kuondoka na angalau pointi moja.
Kati ya mechi nane za Jumatano, Manchester
United pia ilikuwa uwanjani kupambana na Galatasaray, na vijana wa Sir
Alex Ferguson wakichezea nyumbani, mechi ya kundi G, walipata ushindi wa
bao 1-0.
Michael Carrick aliandikisha bao hilo mapema, dakika ya 7.
Klabu hiyo ya Uturuki itadhaniwa na wengi kwamba
ilinyimwa nafasi ya kusawazisha, kwa mwamuzi kuwapa penalti, baada ya
Nemanja Vidic kumchezea vibaya Umut Bulup.
No comments:
Post a Comment