Wiki hii Ney wa Mitego amekuwa gumzo la nchi kwenye upande wa Bongo Movies. Katika kipindi cha Take One cha Clouds TV kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema kila jumanne, Ney amefichua masuala mazito ya jinsi baadhi ya waigizaji wa kike wa filamu nchini wanavyojiuza. Suala hilo ndilo lililopelekea awachane kwenye ‘Nasema Nao’.
Msanii huyo asiyeogopa kuwachana watu maarufu pale anapoona wanazingua, alisema alikuwa na mshikaji wake wa karibu ambaye alikuwa anampenda msichana mmoja wa Bongo Movie. Kutokana na mapenzi yake kwa msichana huyo jamaa huyo alikuwa akinunua kila movie yake hata kama ikiwa mbaya.
Kuna siku walitoka kwenda klabu moja na mshikaji huyo na kama bahati wakakutana na mrembo huyo. Mshakaji wake aliupiga moyo konde na kwenda kuongea naye bila kujali kama atatoswa ama vipi. Ney anasema haikuwa rahisi lakini baadaye yule msichana alimwelewa na akamwambia hisia zake.
“Kitu cha kwanza kabisa alimuuliza una hela wewe? Yaani ikimaanisha kwamba yeye hana mapenzi yeye ni hela, alimuuliza unaniuzia, akasema no wee huwezi kunipenda mimi. Kwahiyo kama unanitaka sababu umeniona kwenye TV nimekuvutia, tuongee tu nipe hela yangu ntakutumizia ndoto yako.”
Ney anasema mshikaji yule alimfuata kumuomba ushauri na kusema kuwa hela aliyoitaka msichana huyo alikuwa nayo nay eye kumwabia afuate hisia zake. Jamaa huyo alimkabidhi muigizaji huyo hela aliyoitaka na kuondoka naye ambapo alipanda kwenye gari ya Ney akawapeleka hotelini na kuwaacha.
Baada ya tukio hilo, Ney na mshikaji wake waliamua kufanya utafiti ili kujua kama ni tabIa ya wasichana wengi wa Bongo movies na baada ya wiki moja walimtafuta mwingine. “Naye picha lilikuwa lilelile, kila mtu ana kiwango chake”, alisema Ney.
“Ngoja niwaambie, wewe uliepo kitaani yaani, hebu changa pesa zako nini ukifikia kwenye laki tano au nne…. sababu msichana wa kwanza nakumbuka jamaa alimpa kama laki tano hivi akalala naye mpaka asubuhi, wa pili ambaye mimi nampendaga kwenye movie yaani nikimwangalia hivi huwa najisikia raha, lakini kwa kilichotokea nikabaki kwamba nampenda kwenye movie tu, nikivuta matukio yake tofauti na movie namchukia, sababu wanajirahisisha kihivyo, alipewa laki tatu tu. Kuna msichana wa tatu alidai dola elfu moja lakini mwisho wa siku naye alipewa laki sita.”
Ney anasema ndipo alipoamua kuzungumza kitu hicho na awali alipanga kufanya wimbo mzima kuhusu ukahaba unaofanywa na wasichana wa Bongo Movies lakini aliamua tu kukipachika kwenye ‘Nasema Nao.
Amesema wasichana zaidi ya asilimia 80 wa Bongo Movies wako hivyo ambapo huingia kwenye fani hiyo ili kupata soko kutoka kwa wadau wa mjini ambao huwatumia kimwili.
Amewataka wasichana wa movie wabadilike ili kusafisha jina la tasnia ya filamu nchini. “Wasafishe ule uchafu uliopo, ili wananchi wakae waseme tunaangalia movie.”
No comments:
Post a Comment