Mwalimu Daniel Urioh. |
Ninaomba
WIZARA YA ELIMU iwe makini na wawekezaji katika secta ya elimu, hasa
kwenye shule ambazo zinatoa msaada kwa watoto wakitanzania ambao familia
zao hazina uwezo wa kifedha, kwa mfano ninaomba mmiliki wa shule ya St
Jude apate muda wa kusikiliza kilio cha wafanyakazi wake wakitanzania
kwani kimsingi wamekuwa wakiteswa, kukandamizwa na kupuuzwa wanapodai
haki na maslahi bora kazini kwao.
Shule
hii utumia picha za wafanyakazi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedha
kuendesha shule, kwa wafanyakazi na wanafunzi hupigwa picha mara kwa
mara na kulazimishwa kuleta picha za familia zao kila mwaka bila shule
kuweka wazi kwa mfanyakazi kuwa anawafadhili wangapi, wafadhili
huchangia kiasi gani cha fedha, kukatazwa kuwasiliana na mfadhili,
kuruhusiwa kuhoji lolote kuhusu pato na matumizi ya uzalishwaji wa fedha
kupitia wewe na familia yako? Hata hivyo picha za familia zinazalisha
fedha kwaajili ya uendeshaji wa shule ilihali familia haifaidiki kwa
uuzaji huo wa sura zao ughaibuni? Kinachosikitisha zidi ni pale
mfanyakazi anapoachishwa ,shule inaendelea kitumia picha za wafanya kazi
na familia zao kuzalisha fedha nyingi za kigeni bila ridhaa wala fedha
hizo kuwafaidisha wenye picha, na kutojali kuwa kitendo hicho kinyume na
sheria.
Pia
picha hizo zimekuwa mara kadhaa zikidhalilisha utu na uhuru wa
muafrika, kwani sura za watanzania zimekuwa bidhaa ya kuzalisha fedha
zisizojulikana ni kiasi gani na kwa faida ya nani? tena ulazimisha
vitendo visivyo halisi na maisha yetu mfano unalazimishwa kucheka
ukichukuliwa picha ilihali mapato uzalishayo hujui na ukikataa
kutekeleza unatishiwa kufukuzwa kazi, wanafunzi ushikishwa zawadi
zisikuwa zao na kupigwa picha na uzalisha kiasi cha fedha bila ridhaa
wafunzi wanapohoji hupewa adhabu au kutishiwa kufukuzwa.
Kama
hiyo aitoshi shule hii imekuwa mara kadhaa ikipuuza sheria za nchi bila
sababu za msingi mfano wamekuwa wakiajiri familia za ughaibuni kinyume
na sheria za nchi mfano wanaajiri baba, mama na mtoto wa familia moja
tena kwenye nafasi za juu na kutoweka wazi taaluma zao wakiwaaminisha
kuwa ukiwa mzungu basi we msomi wa kila kitu, kinyume na sheria ya ajira
nchini, pia shule imekuwa mara kadhaa haieshimu sikukuu za kitaifa bila
sababu za lazima na kutojali wala kuthamini mchango wa waasisi na
wazalendo waliopoteza maisha kujenga utaifa, amani na umoja wa Tanzania,
cha kushangaza shule ujiamulia siku za mapumziko ya wafanyakazi na
wanafunzi watakavyo wao, huwa najiuliza hivi shida inaweza tulazimisha
kufuata sheria za wawekezaji na kupuuza sheria za nchi yetu Tanzania?
Linalosikitisha
zaidi shule hii imekuwa hodari wa kupiga vita ya matumizi ya lugha ya
kishwahili kwa wanafunzi na wafanyakazi hata kudiriki kuwaadhibu kwa
kuwarudisha wanafunzi nyumbani kwa kosa la kuzunguza kishwahili, hata
kufika mbali zaidi na kufukuza mwalimu mwenye shahada ya ualimu kwa kosa
ni kuzungumza kishwahili na wanafunzi, huu ni uvunjaji wa sheria za
nchi usiovumilika.
Hata
hivyo nataka wao wajue kuwa lugha ya taifa Kiswahili imekuwa mhimili
mkubwa wa kujenga umoja na amani. Kiasi cha kuwa wekeza kupata
mafanikio, kama awa amini wakajaribu kuwekeza Somalia na kuwasaidie
watoto wa Somalia wenye shida kubwa ya elimu, ilo linge ondoa jeuri yao
ya kupuuza sheria za Tanzania.
Kitendo
cha shule hii kuwatumia watanzania kama bidhaa na utaratibu wao wa
fukuza fukuza waliyonayo hasa kwa watanzania. Shule hii huwatumia
viongozi wazalendo kuwanyanyasa wenzao na kusaidia shule kuendelea na
dharau na kupuuza sheria za nchi zenye maslahi kwa wazalendo, wale wote
watakaonyesha uzalendo kama mimi wakuonyesha kukerwa na kuchukua hatua
ya kuhoji na kutetea sheria za nchi na watanzania dhidi ya upuuzwaji wa
uzalendo, haki, utu, lugha ya taifa, maslahi ya kiwango cha
utumikishwaji, niliishia kufukuzwa kwa kosa la kuongea kishahili na
wanafunzi.
Ushauri wangu kwa wizara ya elimu.
Kwanza
kupandisha mshahara na mazingira ya kazi serikalini ilikuvutia waalimu
wote toka shule binafsi kwani wangi wamechoshwa ni manyanyaso ya
waajiri.
Pili
kufanya ukagua si wa taaluma tu bali pia mfumo wa uajiri na maslahi ya
watanzania waajiriwa kwenye shule zinazomilikiwa binafsi kwa misaada ya
watu toka ughaibuni.
Tatu
iwe na utaratibu wa ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya shule
zinazopata fedha toka kwa wafadhili kwani shida za watanzania zimekuwa
zikinufaisha wachache na kutengeneza ajira ya watu wasiona sifa za
kufanya kazi ughaibuni na kuja kufanya kazi ambazo wazalendo wanaweza
kuzifanya.
Nne
kusisitiza hasa shule binafsi nchini kuthamini lugha ya kishwahili,
kuheshimu sheria za ajira, kuheshimu sikukuu za kitaifa na kuheshimu,
kulinda tamaduni na vipaji vya watanzania kwa manufaa ya Tanzania.
Ni kweli tar 15/06/2012 nimefukuzwa kazi ya kufundisha (ualimu) St-Jude-Arusha kwa kosa la kuzungumza Kiswahili.
Uzalendo gharama nimeamua kujitoa kwa kutetea nchi yangu Tanzania.
Mwalimu Daniel Urioh. Kwa undani zaidi piga :+255 755 379 737.
No comments:
Post a Comment