Askari
wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Morogoro akipokea maelezo
kutoka kwa abiria wawili akiwemo mwanajeshi waliokuwa ndani ya basi la
Ally's lenye namba za usajili T 692 BKV lililopata ajali katika kijiji
cha Makunganya Wilaya ya Mvomero mkoani hapa wakati likitokea jijini Dar
es Salaam kuelekea jijini Mwanza leo.
Abiria, Tatu Anthony akiangua kilio baada ya kunusurika kwenye ajali ya basi la Ally's.
Abiria huyu alinaswa na mtandao huu akitoa mizigo yake kupitia tundu la kuingiza hewa katika basi la Ally's.
Abiria akiwa na watoto wake wawili ambao wote walinusurika kwenye ajali ya basi la Ally's.
Basi la Summry nalo likiwa limeacha njia katika eneo hilo hilo la kijiji cha Makunganya Wilaya ya Mvomero mkoani hapa.
Mkuu
wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka (kushoto) ambaye ajali hizo tatu
zimetokea kwenye wilaya yake akifarijiwa na Meya wa Halmashuri ya
Manispaa ya Morogoro, Amir Juma Nondo (kulia) katika eneo la ajali.
----
MABASI matatu yamepata ajali leo katika kijiji cha Makunganya Wilaya ya Mvomero mkoani hapa, huku chanzo kikielezwa kuwa ni barabara kuteleza kufuatia mvua kubwa iliyonyesha asubuhi ya leo. Mabasi hayo yaliyopata ajali ni basi la Ally's na Summry yote yakiwa njiani kuelekea Mwanza yakitokea jijini Dar es Salaam na basi la Shabiby lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro (RTO), Leonard Gyndo alipohojiwa na mwandishi wetu eneo hilo la tukio alipingana na kauli ya habari hiyo akidai kuwa chanzo cha ajali hizo ni mwendo kasi wa mabasi hayo.
"Kama suala ni utelezi, basi magari yote yangeanguka eneo hili, mbona magari mengine yanapita salama licha ya barabara hii kulowa kwa mvua? ieleweka kuwa mabasi haya kila moja limeanguka kwa wakati wake ingawa yote yalianguka kwenye eneo moja" alisema RTO, Gyndo.
Bw. Gyndo aliongeza kuwa katika ajali hizo tatu hakuna mtu aliyepoteza maisha ingawa kuna majeruhi kadhaa wamekimbizwa hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu.

Mwandishi wa habari hizi alipofika eneo la tukio alikuta tayari basi la Shabiby limeshaondolea eneo hilo.
No comments:
Post a Comment