SIKU moja baada ya kuvamiwa na wezi nyumbani kwake, Jeti Lumo,
Temeke, jijini Dar na kukombwa vitu kibao, staa wa sinema za Bongo,
Kulwa Kikumba ‘Dude’ amemrejeshea fedha zake mwimba Injili, Felix Ilomo
baada ya kumbana sana.
Wiki iliyopita, Ilomo alisema anajiandaa kumpandisha Dude kizimbani
endapo angeendelea kumzungusha na fedha zake kiasi cha shilingi milioni
nne (4,000,000) alizompa kwa ajili ya kumsaidia maandalizi ya kushuti
video ya wimbo wa Kwa Neema Yako Yesu.
Ilomo alidai kuwa alimkabidhi fedha hizo Dude tangu mwanzoni mwa
mwaka huu lakini kila akiulizia siku ya kushuti video hiyo, msanii huyo
alikuwa akimzungusha na kumwambia mtu wa kufanya kazi hiyo alisafiri nje
ya Jiji la Dar.
Paparazi wetu alipompata Dude kwa njia ya simu alikiri kurejesha
fedha hizo lakini akasema si kwa sababu ya kutishiwa kupandishwa kortini
bali alilipa kwa hiari yake kwa vile yeye alikuwa muunganisha mipango
na si mtendaji, hivyo hata kama angeacha asingeathirika chochote.
“Nimeona nimpe tu fedha zake ndugu yangu huyu mtumishi wa Mungu
lakini ukweli ni kwamba fedha nilimkabidhi George ambaye ndiye alikuwa
amfanyie video yake ila kwa sababu ameshindwa kumvumilia acha nimlipe
mimi halafu George akirudi Dar atanirejeshea,” alisema Dude.
Usiku wa kuamkia Jumatano ya Agosti 8, 2012, Dude aliingiliwa na majambazi nyumbani kwake ambako waliiba samani kadhaa.
Kwa mujibu wa Dude mwenyewe, yeye alikuwa ‘lokesheni’ kwa ajili ya kurekodi filamu ila familia yake, yaani mkewe (Eva) na watoto walikuwepo.
Kwa mujibu wa Dude mwenyewe, yeye alikuwa ‘lokesheni’ kwa ajili ya kurekodi filamu ila familia yake, yaani mkewe (Eva) na watoto walikuwepo.
Alisema wezi hao walipuliza dawa inayosadikiwa ni ya kumfanya mtu
alale fofofo na ndipo walipopata nafasi ya kuvunja milango na kukomba
vitu.
Alisema ameshafungua kesi kwenye Kituo cha Polisi cha Jeti Lumo ambapo msako mkali wa kuwanasa wezi hao unaendelea.
No comments:
Post a Comment