Zikiwa hata wiki mbili
hazijaisha toka mke wa zamani wa mwimbaji Usher Raymond Tameka Raymond
kumzika mwanae kipenzi Kile aliefariki dunia kwenye ajali iliyotokana na
pikipiki zinazoendeshwa kwenye maji, Mama huyu wa watoto watano ametoa
kauli ya kwanza toka msiba utokee.
Tameka ambae kwa kipindi kirefu
amekua mahakamani kutokana na kesi ya kugawana watoto yeye na mumewe wa
zamani Usher Raymond, amesema hii statement haijaandikwa na timu yake,
msaidizi wake wala yeyote bali ni maneno ambayo ameyaandika kutoka
moyoni mwake.
Ripoti yake inasema hivi “Kwa
majonzi makubwa nimejikuta nikilazimika kujibu waraka wa mahakama
unaonitaka nifike Mahakamani kwenye kesi ambayo sio mimi niliyeianzisha,
sikumshitaki mtu yeyote kwenye hii kesi ya January 2011 japo
niliridhika na maamuzi ya ya kugawana majukumu kuwalea watoto”
“Kinachonisikitisha ni
kulazimika kwenda Mahakamani katika kipindi ambacho naomboleza kifo cha
mwanangu, hata hivyo sitozuia Mahakama kufanya kazi yake, nitaendelea na
yale yote nitakayolazimika kuyafanya huku nikiwa na matumaini kuwa hali
hii ngumu itanisaidia kupambana na hali nyingine ngumu zaidi ya majonzi
ya mwanangu” – Tameka
Kwenye line ya mwisho, Tameka
mwenye umri wa miaka 41 amesema “naisihi jamii yote kutoamini yale yote
yanayosikika kwenye vyombo vya habari na pia jamii isiwe nyepesi ya
kuhukumu, wanangu ndio ulimwengu wangu na nitapambana kufa na kupona
kuwalinda na kuwa nao maisha yangu yote”
Hiyo ni taarifa kupitia mtandao
wa Global Grind, Hallo Beautiful wameripoti kwamba Usher Raymond
hakutoa ushirikiano wowote kipindi cha msiba na hakuwahi kuongea na
Tameka wala familia yake, pia alikwenda kumzika Kile kwa sababu tu
tayari anajulikana kwamba ni mtoto wake wa kufikia na vyombo vya habari
na watu wengine walitegemea kuona angefanyaje kwenye maziko ya mtoto wa
mke wake wa zamani.
HBL wameripoti zaidi kwamba
taarifa zilizopo ni kwamba wakati wote wa msiba Usher alikua hapokei
simu za Tameka wakati alipohitajika kutoa msaada wa pesa kwa ajili ya
matibabu ya Kile alipokua
No comments:
Post a Comment