Waziri wa ulinzi wa Syria
pamoja na naibu wake wameuawa katika shambulizi la kujitoa mhanga
lililofanywa dhidi ya makao makuu ya ulinzi mjini Damascus.
Taarifa hizi ni kwa mujibu wa runinga ya kitaifa nchini Syria.
Daoud
Rajiha aliyekuwa shameji ya rais Bashar Al Asaad pamoja na naibu wake
Assef Shawkat walikuwa wanahudhuria mkutano wa maafisa wakuu wa serikali
wakati wa shambulizi.
Afisaa mkuu wa ujasusi pamoja na waziri wa mambo ya ndani wanasemekana kuwa katika hali mahututi.
Shambulizi hili linajiri wakati taarifa zinasema kuwa waasi wanakaribia kuuzingira mji mkuu Damascus.
Shambulizi lenyewe limetafsiriwa kama hatua
kubwa katika mapambano dhidi ya utawala wa rais Assad ambao wapinzani
wanataka kuuangusha.
Hatua ya mshambuliaji wa kujitoa mhanga kuweza
kupenya na kufanya shambulizi kama hili, dhidi ya makao ya ulinzi ya
serikali ya Assad ambayo ulinzi wake unakuwa umedhibitiwa sana.
Shambulizi la leo linazua maswali mengi kuhusu
uwezo wa serikali kulinda maafisa wake na pia kuhusu hali ya usalama wa
serikali ya Syria.
Huku idadi ya maafisa wakuu wanaojiuzulu kutoka
kwa serikali ya Syria ikiongezeka, wadadisi wengi wanaamini kuwa kwa
sasa hakuna nafasi kwa swali la ikiwa serikali ya Syria itaporomoka
kuanzania ndani bali ni lini tu itakapoporomoka.
Wakati jeshi pamoja na zana zake nzito mfano
vifaru na ndege za kivita, likiwa bado lina uwezo mkubwa wa nguvu dhidi
ya upinzani, kuna dalili kuwa linakabiliwa na changamoto kubwa katika
mashambulizi ya ardhini.
Hata hivyo wafuasi wa rais Assad wa madhhebu ya
Alawite hawana pa kwenda. Hali hii inazua hofu ya kuchochea aapigano ya
kikabila yanayoendelea nchini humo ikiwa rais Assad atangolewa
madarakani.
No comments:
Post a Comment