Naomba kusema kwamba AY atakua
msanii mwenye bahati sana, na hili nalisema kutokana na stori mpya
nilizopata kutoka kwenye kinywa cha Jose Chameleone wa Uganda.
Najua unajua kwamba SEAN
KINGSTON alipokuja Tanzania alisema anatambua kazi za AY ambapo siku
chache baadae AY alitangaza kwamba KINGSTON amekubali kufanya nae kolabo
bila kumtoza pesa yoyote, kolabo ambayo ipo hata demo yake nilipewa
nikaisikiliza japo bado single haijatoka mpaka sasa.
Tuje kwenye kilichonifanya
niandike hayo yote hapo juu, stori ni kwamba Staa wa muziki kutoka
Uganda Jose Chameleone anafanya kolabo na Sean Kingston lakini
analazimika kumlipa.
Exclusive na millardayo.com
Chameleone amesema “narekodi album yangu mpya ambayo ina single kama
Valu Valu inaitwa Extra Chameleone, meneja wangu wa Canada ameshaongea
na uongozi wa Sean Kingston na amekubali kufanya kolabo lakini bado
haijapatikana time ya kufanya video.. mimi kuimba na Sean Kingston na
hatujafanya video haita saidia chochote, na kwa kolabo hiyo ya audio na
video ninalazimika kumlipa dola za kimarekani elfu 30 ambazo ni zaidi ya
milioni 45 za kitanzania”
Kwa kauli hiyo Jose Chameleone
amethibitisha kwamba SEAN KINGSTON ndio atakua msanii wa kwanza kumlipa
kwa ajili tu ya kufanya nae kolabo ndio maana nilisema ni bahati kwa Ay
ambae amepewa nafasi ya bure kufanya kolabo na Kingston, na
kilichomfanya pia apate shavu la kufanya kolabo na Romeo Miller na
Lamyia ilikua ni baada ya kina Romeo kusikia demo ya kolabo ya Kingston
na Ay kwenye studio huko Marekani, ndio wakavutiwa kupiga nae kolabo
pia.
Umeonaje hii story, kama umeipenda like au tweet na rafiki zako waione pia.
No comments:
Post a Comment