Uchina imeandikisha ukuaji wa uchumi mdogo zaidi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotolewa na
serikali ya nchi hiyo, uchumi wa uchina ambao ndio wa pili kwa ukubwa
duniani ulikuwa kwa asilimia saba nukta sita katika robo ya pili ya
mwaka huu, hii ikiwa ni asilimia moja nukta nne chini ya kiwango
kilichoafikiwa katika robo ya kwanza mwaka huu.
Kuanguka huko kwa uchumi kunasemekana ni sababu ya kupungua kwa mauzo ya nje na watu kubana matumizi yao ndani ya China.
Mwandishi wa BBC mjini Beijing anasema kuwa
viongozi wa china wameweka matumaini yao katika kuvuta uwekezaji mpya
ili kuchochea kukuwa tena kwa uchumi.
No comments:
Post a Comment