Serikali ya Tanzania imetangaza
kulifungia gazeti la MWANAHALISI kwa muda usiojulikana kutokana na
kuandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi likiwa na nia
ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola.
Taarifa iliyotumwa kwenye
vyombo vya habari na ofisi ya msajili wa Magazeti Wizara ya habari,
Vijana, Utamaduni na michezo imesema katika matoleo ya hivi karibuni,
gazeti hilo limekua likichapicha habari na makala zenye kueneza na
kujenga hofu kwa wananchi.
Taarifa imesema kabla ya uamuzi
wa kulifungia Mwanahalisi, mhariri wa gazeti hilo aliitwa na kuonywa
mara nyingi lakini hakuwa tayari kukiri kuwa maudhui ya makala zake
hayakua na tija kwa jamii na zilikua hazifati madili ya uandishi wa
habari japo amekua akinukuu kifungu cha 18 cha katiba ya Uhuru wa kutoa
maoni ambapo hii ni mara ya pili kufungiwa, kabla liliwahi kufungiwa kwa
miezi mitatu.
Unaweza kulike au kutweet hii post ili na wenzako waione.
No comments:
Post a Comment