BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Tuesday, July 3, 2012

STORI KAMILI YA BINTI WA MIAKA 14 ALIYEMUUA BABA YAKE NA KAKA KWA MAKUSUDI.

Huyu ni mzee ambae nae zaidi ya wiki mbili zilizopita alimuua mwanae wa kike kwa kumkata panga shingoni kwa sababu amekua kwenye mapenzi na mwanaume asimtaka.
Polisi wa India wamemkamata binti wa miaka 14 ambae amemuua baba yake mzazi na kaka yake kwa sababu walikua wanapinga uhusiano wake wa kimapenzi na mvulana ambae anatokea kwenye familia ya kimasikini zaidi yao.
Shirika la habari la AP limeripoti kwamba Mtoto huyo amewaambia polisi alichanganya sumu na mboga alizokua amewapikia familia yake nyumbani jumamosi iliyopita.
Mama yake mzazi ambae ni Sunita Devi amesema ameepuka kifo kwa sababu alikua anaumwa na alikataa kula hicho chakula kwa sababu ya kuumwa lakini hakushtukia mchezo wa mtoto huyo ambae boyfriend wake alishawahi kupigwa na hiyo familia siku walipoonekana wakiwa kwenye pozi za kimapenz.
AP wameripoti kwamba Visa kama hivi hua vinatokea sana nchini India kati ya familia tajiri na zile maskini, ambavyo mara nyingi familia za kitajiri huonyesha kama wanadhalilishwa na watoto wao kwa kua na uhusuano wa kimapenzi na watu wa familia masikini, ambapo inasemekana takriban watu 900 huuawa kila mwaka kwenye miji ya kaskazini ya Haryana, Punjab na Utta Pradesh.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...