Kampuni ya Samsung Tanzania, imezindua simu ya Samsung Galax Pocket
yenye uwezo wa kufukuza mbu usiku, pindi mtumiaji anapowasha.
Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam na Mwanafunzi wa Chuo cha
Elimu ya Biashara (CBE), Belinda Lawuo ambaye ni miongoni mwa watumiaji
watano waliopata fursa ya kutumia simu hiyo siku chache kabla ya
uzinduzi uliofanyika juzi.
Lawuo alisema alipopata simu hiyo alifurahishwa na uwezo wake wa kufukuza mbu kupitia programu ya Mosquito Repellant.
Naye Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania, Kishor Kumar alisema simu hiyo
inampa mnunuzi thamani halisi ya pesa, kwani inauzwa bei nafuu, huku
kukiwa na ofa mbalimbali, ikiwemo kutuma ujumbe bure mara 100 kwa mwezi
na kifurushi cha intaneti
watu wanachangamkia kinomaaa mi nishaidownload kwa sumsung yangu, vipi iphone itakubali?
ReplyDelete