BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Saturday, July 7, 2012

SAKATA LA ROSE, JINI KABULA CHUZ AKIMBILIA POLISI

Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.

Rose Michael.
Tuesday Kihangala ‘Chuz’.
SIKU chache baada ya uchumba kati ya Mkurugenzi wa Chuz Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ na msanii wake, Rose Michael kuvunjika, tayari bosi huyo amekimbilia Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar kufungua mashitaka.
HABARI MEZANI
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Chuz alikwenda polisi aliposikia Rose ametua jijini Dar akitokea kwao Arusha na wasichana wengine watano kwa lengo la kumshikisha adabu mzazi mwenzake na Chuz, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye siku chache zilizopita walitibuana.
“Rose ametua Dar na wasichana watano, wamefikia kwenye gesti moja Mabibo. Lengo lake anataka kumfanyia fujo Jini Kabula maana yeye ndiye chanzo cha uchumba wake na Chuz kuvunjika kwa madai alikuwa anamtesa mwanaye.
“Sasa Chuz baada ya kusikia hilo amekwenda kuripoti polisi, maana anahisi linaweza kutokea lolote yeye akawa ndiyo chanzo, akakamatwa,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata taarifa hiyo, Risasi Jumamosi lilimwendea hewani Chuz na kumuuliza kuhusu madai hayo, ambapo alitoa ushirikiano.

MSIKIE CHUZ
“Ni kweli Rose amekuja Dar, nasikia kaja na kundi la mademu kwa lengo la kumpiga Jini Kabula. Sasa katika hali kama hii ilinilazimu niende kuripoti Oysterbay (kituo cha polisi), maana kuna leo na kesho.
“Niliposikia amekuja na hao wasichana na lengo lao ni kumsaka Jini Kabula niliamua kumpigia ili nimuonye kuachana na zoezi lake, lakini hapatikani.”
Rose hakupatikana hewani siku ya Alhamisi (juzi) ili kuzungumzia madai hayo, lakini Jini Kabula alipopatikana kwa simu alisema yuko tayari kwa mapambano kati yake na Zambarau.
“Yeah! Nimesikia dogo (Rose) karudi Dar ili anioneshe kazi, lakini niko tayari, wala hakuna tatizo, aje tu,” alisema Jini Kabula.

KISA KILIANZAJE?
Awali, Chuz akiwa Zanzibar alipokuwa anarekodi filamu yake mpya, alipewa taarifa kwamba Jini Kabula alikwenda nyumbani kwake Makongo, Dar na kumfanyia fujo Rose akidai mwanamke huyo anamtesa mwanaye.
Kufuatia hali hiyo, Chuz aliporudi, Rose aliamua kuondoka kwa mwanaume huyo na kwenda kwa wazazi wake Arusha mpaka juzi ilipodaiwa amerejea Dar kwa lengo la kumfanyia mashambulizi Jini Kabula.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...