Chama cha FA kimempa hadi tarehe 2 Agosti kujitetea
Chama cha kandanda cha FA nchini
Uingereza, kimeelezea kwamba kitamshitaki mchezaji wa Manchester
United, Rio Ferdinand, kufuatia maandishi yake katika mtandao wa kijamii
wa Twitter.
Ferdinand alikanusha habari kwamba yeye ni
mbaguzi wa rangi, kufuatia maneno yake kuhusiana na "choc ice",
akimaanisha barafu ya kula yenye rangi mbili, katika kuelezea mchezaji
wa Chelsea, Ashley Cole, ni mtu wa aina gani.
"Choc
ice" ni maneno ambayo hutumia kuelezea juu ya rangi nyeusi na nyeupe
katika barafu hiyo, na ni maneno yanayoweza kutumiwa katika kuelezea
kwamba mtu fulani juujuu ni mweusi, lakini ndani hasa yeye ni mweupe.
Ferdinand, mwenye umri wa miaka 33, ana muda wa kujitetea, hadi saa kumi, tarehe 2 Agosti, kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi.
Taarifa katika mtandao wa FA inaelezea: "Madai
ni kwamba mchezaji huyu alionyesha tabia isiyokuwa nzuri/na kwa njia
inayouletea mchezo fedheha kwa kuandika maneno hayo kuhusu asili au
rangi."
Cole, ambaye ni mchezaji wa ulinzi wa Chelsea,
alifika mahakamani kama shahidi wakati wa kumtetea mchezaji mwenzake
katika timu, John Terry, na ambaye mahakama ilimuondolea mashtaka
kuhusiana na ubaguzi wa rangi.
Terry alikuwa ameshtakiwa kwa kutumia matamshi
ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mdogo wake Ferdinand, Anton, katika mechi
iliyochezwa tarehe 23 Oktoba mwaka jana.
Terry, mwenye umri wa miaka 31, tayari
ameshtakiwa na chama cha FA kwa tabia isiyofaa, dhidi ya Anton
Ferdinand, na ameapa kujitetea kuhusiana na madai hayo.
No comments:
Post a Comment