BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Monday, July 2, 2012

NDOA YA MISS TZ, SIRI YAFICHUKA



Husna Maulid akiwa na Abubakar siku ya ndoa yao.

NDOA ya mshiriki wa kinyang’anyiro cha Miss Tanzania 2011, Husna Maulid iliyofungwa kisirisiri lakini ikanyakwa na gazeti hili wiki iliyopita, nyuma yake kuna siri ambayo sasa imefichuka, Ijumaa Wikienda lina jipya.
Imebumburuka kuwa mwanaume aliyemuoa Husna siye aliyekuwa akioa bali ilikuwa geresha kwa waalikwa.
Chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu na familia ya Husna kimeeleza kuwa kuwa mwanaume aliyeonekana pichani akiozeshwa siku ya ndoa hakuwa yeye na kwamba aliyestahili kumuoa ni mwingine aliyetajwa kwa jina la Tariq ambaye ndiye aliyemvisha pete ya uchumba.
Chanzo hicho kilieleza kuwa, mwanaume aliyeoa aliyetajwa kwa jina la Abubakar siku hiyo alikwenda kufanikisha tukio hilo tu lakini muoaji sahihi alikuwa Tariq ambaye hakutaka kuwa mhusika mkuu eti kuepusha maneno kutoka kwa watu.
Gazeti hili baada ya kupata mchapo huo, lilimtafuta huyo Tariq ambaye bila kusita alikubali kuwa yeye ndiye mume wa Husna na kukiri kumtuma Abubakar siku hiyo akamuolee Husna.
“Hujakosea, ni kweli mimi ni Tariq, mume wa Husna Maulid. Siku hiyo nilikuwa siko sawa ndiyo maana nikamtuma rafiki yangu wa karibu Abubakar akaniolee kwani kiislamu inaruhusiwa,” alisema jamaa huyo.
Katika sherehe ya tukio hilo hata waalikwa hawakuishtukia ishu hiyo.
Kama weledi unavyotaka, Ijumaa Wikienda lilimgeukia Husna na kumbana kwa nini alificha juu ya mwanaume aliyemuoa ambapo alisema kwa kifupi: “Kwa kifupi eleweni kwamba mume wangu ni Tariq wala si Abubakar.”

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...