Marcus Agius aliamua binafsi kujiuzulu kutokana kwa kile
alichotaja katika taarifa yake ya kujiuzulu kama pigo kubwa linalotokana na
kuharibiwa sifa kwa kampuni hiyo kwa sababu ya madai ya kuwalaghai wateja
kupitia nyongeza haramu ya riba.
Wito umetolewa kuwa afisa mkuu mwandamizi wa kampuni hiyo, Bob Diamond
ajiuzulu, kwa sababu alikuwa akisimamia uwekezaji wa benki hiyo wakati mpango
ulipofanywa kulaghai wateja kupitia kwa riba inayotozwa katika benki hiyo.
Hata hivyo wakurugenzi wa Barclays wameamua kuwa Bwana Diamond ataendelea
kufanya kazi.
Kwa hivyo Bwana Agius, ambaye pia ni mwanachama wa Bodi, aliamua, huku
akiungwa mkono na wenzake, kujitwika lawama zote zinazotokana na madhambi
yanayokabili Benki ya Barclays na hasira yote waliyo nayo wenye hisa wa benki
hiyo.
Mtu anayetazamiwa kuchukua mahali pake ni mkurugenzi mwingine, Sir Mike Rake,
ambaye kwa sasa atalazimika kujiuzulu vyeo vyake vya kuwa mwenyekiti wa Easyjet
na BT.
Naye Bwana Diamond hajajiondoa katika lawama bado kwani atahojiwa na Wabunge
kuhusu mawasiliano ya siri ya mwaka wa 2008 kati yake na naibu wa Gavana wa
Benki Kuu, Paul Tucker.
Meneja wa Barclays wanaamini kuwa ni katika mawasiliano hayo ambapo Benki Kuu
ya Uingereza iliamuru Benki hiyo kudanganya kuhusiana na riba inayotozwa.
Hiyo haikuwa kweli lakini Bwana Diamond atalazimika kuwaeleza Wabunge
anachokumbuka Bwana Tucker akimweleza wakati ule na kile ambacho baadaye
aliwaeleza wafanyakazi wenzake.
Itakuwa aibu kubwa kwao iwapo yeye au Bwana Tucker watagunguliwa kwamba
waliwashawishi wenzao kulaghai kupitia riba haramu.
|
No comments:
Post a Comment