BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Friday, July 27, 2012

Mutula displays 'acceptable' school skirts

STORI  KUHUSU WANAFUNZI WA KIKE KUVAA NGUO FUPI KENYA.

Ishu ya wanafunzi wa kike kuvaa nguo fupi mashuleni Kenya imekua gumzo ambapo Waziri wa elimu Mutula Kilonzo amezungumza leo na waandishi wa habari baada ya watu kuona kwamba anashabikia uvaaji wa nguo fupi kutokana na kauli aliyoitoa siku zilizopita.
Kutokana na hiyo kauli aliyoitoa baada ya wanafunzi kufanya mgomo wakitaka waruhusiwe kuvaa nguo fupi, Makanisa na viongozi wengine wa dini na jamii ya Kenya imemkosoa kwa kusupport kitu ambacho kina haribu maadili.
Kwenye hiyo video hapo chini ndio kuna hizo skirt aina tatu alizozionyesha Waziri Kilonzo.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari leo Kilonzo ameleta mavazi ya aina tatu na kuyaonyesha, alionyesha mavazi ambayo wanafunzi waliyagomea, akaonyesha mavazi ambayo wanafunzi wanayataka na mavazi ambayo yeye aliyapendekeza.
Baada ya hapo alisema watu hawakumuelewa alivyozungumza kwa sababu sio kwamba anaunga mkono bali anapendekeza nguo zisiwe fupi sana.

No comments:

Post a Comment

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...