MTOTO WA MALECELA FUNGA KAZI
William Malecela akiwa katika taswira mbalimbali na warembo kama inavyoonekana pichani juu.
WILLIAM Malecela a.k.a Le Mutuz ambaye anatajwa kuwa ni mtoto wa
mwanasiasa mkongwe Bongo, John Malecela ambaye anadaiwa kuwa ni funga
kazi kwa kupenda kupiga picha na wanawake wazuri kila anapokuwa, Amani
limemfuatilia hatua kwa hatua na sasa linafunguka.
Kwa mujibu wa ‘mapicha’ yake mazuri yaliyopo mitandaoni, asilimia 90 zinamuonesha Le Mutuz akiwa na wanawake wazuri wa kada mbalimbali.

WAMO MASTAA
Mbali na wanasiasa wenzake, Le Mutuz aliyegombea ubunge wa Afrika Mashariki kwa leseni ya CCM hivi karibuni lakini kura hazikutosha, anaonekana kwenye picha nyingi zisizo na idadi akiwa na mastaa mbalimbali wakiwemo waigizaji na wanamuziki wenye majina makubwa Bongo.

NI KILA MAHALI?
Katika picha hizo, Le Mutuz anaonekana akiwa sehemu mbalimbali hasa kwenye kumbi za starehe, baa, migahawani, viwanjani, nyumbani na ufukweni, vyote jijini Dar es Salaam.

ETI NI MAMBO YA ‘KUTOKLEZEA’
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa Le Mutuz, jamaa huyo mwenye ‘sivii’ ya kuishi nchini Marekani kwa muda mrefu amekuwa akiwakaribisha warembo hao kwenye mtandao wake (jina tunalo) kwa kutundika picha hizo na kuwataka waingie humo kujiona ‘walivyotoklezea’.

BAADHI YA MASTAA NI HAWA
Baadhi ya mastaa wanaoonekana na ‘mutu mukubwa’ huyo na kusababisha minong’ono kwa kuwa zina mapozi tata ni pamoja na Wema Isaac Sepetu, Jacqueline Wolper Masawe, Jokate Mwegelo, Miss Tanzania 2011, Salha Israel, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na warembo wengine ‘kibwena’ wasiokuwa na majina.

WAMO MARAFIKI WA FACEBOOK
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, inaelezwa kuwa, Le Mutuz huwa anawasiliana na warembo ambao ni marafiki zake katika mtandao wa kijamii wa Facebook ambapo hukutana nao na kupiga picha ili kuziweka mtandaoni kwake.

MSHANGAO!
Kwa mujibu wa maoni ya watu wanaotembelea mtandao wake wanashangazwa na ishu hiyo huku wakihoji mbona anafanya na mademu tu, tena wazuri?

LENGO NI NINI?
Ili kupata undani wa kwa nini Le Mutuz anafanya hivyo, Amani lilifanya jitihada za kupata kupitia kilongalonga chake cha kiganjani lakini hakupatika, hata hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.

No comments:
Post a Comment