Msichana muogeleaji wa China Ye
Shiwen hajatumia dawa kwenye michezo, mwenyekiti wa Kamati ya Olympiki
Uingereza. Amesema hayo baada ya kocha wa Marekani kuonyesha wasiwasi wa
kuvunja kwake rekodi ya dunia katika mshindano ya kuogelea.
Mwenyekiti huyo Lord Colin Moynihan amesema Ye,
mwenye umri wa miaka 16, alipitia hatua zote za kupimwa kama anatumia
dawa hizo na kukutwa kuwa ni safi na anastahili kutambuliwa kwa kipaji
chake.
Ye alivunja rekodi yake mwenyewe kwa sekunde tano katika mita 400 Medley.
Kocha mwandamizi wa Marekani John Leonard
alisema kufanikiwa kwa binti huyo kulikuwa na mashaka huenda kulikuwa
udanganyifu wa kutumia dawa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la makocha wa
mchezo wa kuogelea Bw Leonard amesema kufanikiwa kwa mwanamichezo huyo
wa China kunamkumbusha mashindano ya kuogelea kwa wanawake ya miaka ya
1980 Ujerumani Mashariki waliokuwa wakitumia utaratibu wa udanganyifu.
"Historia katika mchezo wetu itakuwambia kuwa
kila mara tukiona kitu na nitaweka kwenye nukuu kuwa, ‘si rahisi
kuamini, historia inaonyesha inageuka baadaye kuwa udanganyifu
ulihishwa,"aliliambia gazeti la Guardian la Uingereza.
Lakini Ye, ambaye baadaye atamalizia mashindano
ya fainali ya mita 200,amejitetea mwenyewe kwa nguvu na kukana kuwa
hajawahi kutumia dawa zozote.
Mkuu wa kuzuia udanyanyifu wa dawa kwenye
michezo nchini China amesema binti huyo amefanyiwa uchunguzi mara zaidi
ya mia moja tangu alipofika London na hakuna kipimo hata kimoja
kinachoonyesha kuwa alikuwa ametumia dawa.
Waogeleaji wa zamani na washindi wengine wa Olympiki na hata waatalam wamekuwa wakimuunga mkono Ye.
Lord Moynihan ameviambia vyombo vya habari kuwa
kitengo cha kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu kinadhibiti
vilivyo suala hilo kwenye michezo hii ya Olympic
"Amepitia kwenye mpango wa Wada kwa hiyo yuko
safi. Huu ndio mwisho wa habair hii. Ye Shiwen anastahili kwa kipaji
chake." Alisema.
Mwenyekiti wa Kamati ya Olympic Marekani (USOC)
amejitenga na maoni ya Bw Leonard na Patrick Sandusky, msemaji wa kamati
ya Marekani ameiambia BBC kuwa Wamarekani wanajaribu kumaliza mambo
haya na China kwa utaratibu mzuri.
Mmoja wa wajumbe wa wa timu ya uhusiano wa
kimataifa ya USOC anatarajiwa kukutana na kamati ya Olympic ya China
baadaye Jumanne, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC David Bond.
No comments:
Post a Comment