Ombi la raia wanne mashujaa
wa uhuru wa Kenya kutaka kukubaliwa kufungua kesi dhidi ya wakoloni wa
Uingereza limeanza kusikilizwa katika mahakama kuu ya Uingereza London.
Wanne hao ni pamoja na Paulo Nzilu, Wambugu wa Nyingi, Jane Muthoni
Mara na jamii ya Susan Ngondi.
Mashujaa hao wa uhuru wa Kenya wanasema serikali
ya Uingereza sharti ikiri kwamba maafisa wake walitekeleza dhuluma za
kibinadamu katika iliyokua Koloni yake ya Kenya Afrika Mashariki.
Wamesema kwamba serikali ya ukoloni katika miaka ya hamsini ilitangaza
sheria ya hatari ambapo pia Vuguvugu la mau mau lilitangazwa kua la
kigaidi na raia walioshukiwa kuwa wanachama walipelekwa katika vizuizi.
Wanavijiji
Wengi kutoka jamii za Gikuyu, Embu, Meru na Kamba walikamatwa na
maafisa wa kikoloni kwa kushukiwa kuunga au kuua wanachama wa Mau Mau na
kuwekwa kizuizini ambapo walipitia dhuluma zikiwemo wanaume kuhakisa,
ubakaji wa wanawake na mateso mengine.
Chini ya sheria za Uingereza, mtu hawezi
kuwasilisha kesi katika mahakama zake inayohusisha matukio yaliyofanyika
zaidi ya miaka sita. Hata hivyo mahakama inaweza kuridhia kesi
iliyopita miaka sita kusikilizwa kulingana na uzito na matukio ya kesi
hiyo.
Mashujaa wa Mau mau wamesisitiza kwamba dhuluma
walizopitia ziangaziwe chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu ambayo
ilichunguza kesi katika mauaji ya Ki- Nazi pamoja na uhalifu wa kivita
kufuatia vita vya uliyokua muungano wa Kosovieti.
Baada ya hoja hizi Mahakama kuu ya Uingereza
itaamua ikiwa wazee hawa wanaweza kufungua kesi dhidi ya serikali ya
Uingereza kufuatia dhuluma wakati wa harakati za Uhuru.
No comments:
Post a Comment