Shirika la Msalaba Mwekundu la
Kenya, linasema kuwa watu zaidi ya 20,000 wamekimbilia Kenya, baada ya
mapambano katika mji ulioko kwenye mpaka wa Ethiopia na Kenya.
Mapigano yalianza Jumatano, baina ya makabila mawili, karibu na mji wa Moyale.
Inafikiriwa kuwa watu kama 18 wameuwawa.
Taarifa kutoka eneo hilo zinasema hali sasa imedhibitiwa.
Mapigano yalianza kati ya juma, na chanzo kilikuwa mzozo wa muda mrefu kuhusu ardhi baina ya makabila mawili.
Taarifa kutoka huko zinaeleza kuwa wanamgambo
waliokuwa na silaha walijizatiti Jumatano, na mapigano yakatapakaa
haraka hadi mji wa mpakani, Moyale.
Aliyeshuhudia tukio hilo aliiambia BBC kwamba wanajeshi wa serikali ya Ethiopia waliingilia kati kuzima fujo siku ya Ijumaa.
Lakini ingawa viongozi wa eneo hilo wamewaomba
watu warudi makwao, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya linasema watu
wengi bado wanavuka mpaka na kuingia Kenya.
No comments:
Post a Comment