KOCHA Mkuu wa Atletico, Kazee Cerbric, amesema amefurahishwa na
kiwango cha kipa namba moja wa Yanga, Yaw Berko huku akipiga hesabu za
kuondoka naye.
Kauli hiyo ameitoa muda mchache baada ya mechi dhidi ya Yanga, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar na kumalizika kwa Yanga kufungwa mabao 2-0.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Cerbric alisema ataushawishi uongozi wa juu wa timu yake ili kuhakikisha unamnasa kipa huyo raia wa Ghana.
Cerbric alisema kipa huyo ana vigezo vyote vya kuwa bora, hata umbile na umakini wake ndani ya uwanja, ni vitu ambavyo Yanga inatakiwa kujivunia.
“Nimeuona uwezo wa kipa wa Yanga, ana kiwango kikubwa na ana vigezo vyote vya kuwa bora kutokana na umbile kubwa la kuwatisha washambuliaji wa timu pinzani.
“Nitafanya jitihada zote za kumsajili kipa huyo, hivi sasa nina mpango wa kukutana na uongozi kwa ajili ya kuushawishi ili tumpate,” alisema Cerbric.

No comments:
Post a Comment