Mashirika ya kupigania haki za
kibinadamu zimeishutumu serikali ya Kenya kwa kukataa kugharimia kesi
ambayo wapiganaji wa zamani wa Mau Mau wameishitaki serikali ya
Uingereza.
Wapiganaji hao wazamani tayari wamewasili Mjini
London kushitaki wakoloni walioitawala Kenya kwa madai ya kuwatesa
wakati wakipigania uhuru wa Kenya.
Awali serikali ilitangaza kuwa inaunga mkono kesi hiyo ya Mau Mau.
Lakini wakuu wa serikali wameshindwa kueleza ni kwa sababu gani hawagharimii kesi hiyo.
George Morara alihoji kwanini serikali ya Kenya
haitaki kuwasaidi Mau Mau ambao walipigania uhuru wa Kenya wakati
serikali hiyo hiyo sasa inawasaidia wakenya mashuhuri ambao
wameshitakiwa katika mahakama ya uhalifu wa kimataifa-ICC.
Mwanaharakati huyo amesema kuwa ingawa Mau Mau
ilikuwa maarufu katika miaka ya 1950 hadi 60 lakini kuna baadhi ya
viongozi wa serikali wanaohofia kuwa kesi hiyo huenda ikawadhuru
kisiasa.
Mwandishi wa BBC wa Maswala ya Afrika Martin
Plaut anasema imechukua muda mrefu kwa kesi hiyo kufikia hatua ya sasa
na huenda ikachukuwa muda mwengine mrefu zaidi kwa Mau Mau kuthibitisha
madai ya kuteswa na wakoloni wakati wakipigania uhuru wa Kenya.
No comments:
Post a Comment