Baada ya kuwepo malalamiko ya
rushwa kutembea bungeni na kusababisha kuvunjwa kwa kamati ya kudumu ya
bunge ya Nishati na Madini mwishoni mwa wiki iliyopita, baadhi ya
Wabunge wametaka majina ya wenzao wanaojihusisha na rushwa yawekwe wazi
na wafukuzwe bungeni.
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari (CHADEMA) amesema
pamoja na kwamba kamati ya nishati na madini imetajwa moja kwa moja,
zipo kamati nyingine ambazo wabunge wake wanatajwa kuhusika na kuomba
rushwa.
Amesema “zipo kamati kadhaa
zinatuhumiwa kwa rushwa, Mh Spika nilikua naomba muongozo wako kwamba
kwa nini ofisi yako isiamue kuzivuruga kamati kadhaa ambazo zinatuhumiwa
kwa rushwa ikiwemo kamati ya kudumu ya bunge ya Serikali za mitaa
inayoongozwa na Mh. Mrema na Kamati ya kudumu ya bunge ya Mashirika ya
Umma inayoongozwa na Mh. Zitto Kabwe, hii ni kwa sababu wabunge wengi
wamekua wanazikimbilia zile kamati ambazo zina mikataba lakini kamati
kama ya maendeleo ya jamii ya huduma za jamii ambazo zina umuhimu mkubwa
kwenye nchi kwa sababu hazina mikataba zinakimbiwa”
Mbunge wa Lindi mjini Salum
Khalfan na mbunge wa Nkasi kaskazini Ally keissy Mohamed wamelitaka
bunge kuwafukuza bungeni wabunge wote watakaogundulika kula rushwa,
wanataka watajwe kwa sababu sasa hivi wabunge wengine kila wakipita
barabarani wanakosa raha kutokana na hiyo kashfa ya rushwa iliyolichafua
bunge.
Baada ya hayo Naibu Spika wa
bunge Job Ndugai aliomba kamati ya uongozi wenyeviti wa kamati za bunge
kukutana na Spika kulizungumza ili baadae wampe maelekezo zaidi.
No comments:
Post a Comment