JK LAZIMA AWE REFA MECHI YA WABUNGE
Rais Jakaya Kikwete.
MBUNGE wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba amesema kuwa Rais Jakaya
Kikwete ni lazima awe refa wa pambano la wabunge wapenzi wa Simba na
Yanga litakalopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Julai 7,
mwaka huu.
Kauli ya Nchemba aliyoitoa juzi kwa mwandishi wetu inapingana na ile ya Mbunge wa Kigoma Mashariki, Zitto Kabwe ambaye ni mchezaji wa wabunge wa Simba aliyesema kuwa Rais Kikwete hafai kuwa refa wa pambano hilo kwa kuwa ni shabiki mzuri wa Yanga na anaamini kuwa atawapendelea wabunge wa timu anayoishabikia.
“Zitto ni muoga tu, wasubiri kichapo, Rais Kikwete hawezi kutupendelea sisi (Wabunge wapenzi wa Yanga) na ukweli huo utaonekana siku hiyo ya mchezo,” alisema Nchemba.
Pambano la Wabunge wa Simba na Yanga linangojewa kwa hamu kubwa na wapenzi wa soka kwani ni la aina yake na kwa mujibu wa mmoja wa waratibu wa pambano hilo, Luqman Maloto, viingilio vimepangwa kuwa shilingi 10,000 kwa viti maalum (VIP) na shilingi 5,000 kwa viti vya kawaida.
Maloto alisema anaamini pambano hilo litakalofanyika siku ya Usiku wa Matumaini litakuwa kali na la kusisimua kutokana na kila upande kujiandaa vyema. Licha ya mpira wa miguu kutakuwa na burudani mbalimbali uwanjani hapo ambapo mwanamuziki Chamelione wa Uganda na Diamond wa Tanzania watatumbuiza na wapenzi wa ngumi watajionea mchezo huo.

No comments:
Post a Comment