DJ mkongwe nchini, John Dilinga Matlou ‘DJ JD’, leo nae ameweka wazi
utapeli aliowahi kufanyiwa miaka saba iliyopita na mwanamuziki raia wa
Uganda, mwenye hulka ya utapeli, Joseph Mayanja Chameleone.
JD, amewaeleza waandishi wa habari leo, waliokusanyika kwenye Hoteli ya The Atriums kwamba Chameleone siyo mtu mzuri anapokubaliana na mapromota, kwani hata yeye aliwahi kumtapeli dola za kimarekani 3,000, mwaka 2005.

Alisema mbele ya waandishi wa habari: “Niliwasiliana na Chameleone
moja kwa moja, akanikubalia kwenye tamasha langu lililokuwa linaitwa
Wakilisha. Nilimlipa dola 3,000, baada ya kupokea fedha, hakuonekana
tena na hata simu yangu akawa hapokei.
“Aliendelea kunikimbia hivyo. Tatizo kubwa lipo kwa mapromota wa
Kitanzania, hatuna ushirikiano kabisa. Kila alipokuja nchini kufanya
shoo, nilimfuata promota husika lakini promota mwenyewe alimficha
Chameleone asikamatwe.
“Mwaka 2006, Chameleone alikuja nchini kwenye shoo fulani. Kama kawaida yake alijitahidi sana kujificha nisimfikie. Hata hivyo, pamoja na kujificha kwake, nilipewa taarifa usiku kwamba yupo Bilicanas. Nikawataarifu polisi tukaenda kumkamata.

“Chameleone aliponiaona alinikimbia. Ndugu zangu, Chameleone
alikimbia kama mwizi. Pale Bilicanas walikuwepo Rita Paulsen wa BSS na
Merey Balhabou. Wakati polisi wamemkamata, Chameleone alikubali namdai
dola 3,000 na akakubali kulipa.
“Kusikia hivyo, Rita na Merey wakaniomba nimsamehe kwa sababu mtu
mwenyewe amekubali kulipa. Nikawaambia ameshanisumbua sana, Merey
akasema kama hatalipa, basi yeye atamlipia. Akanisihi sana kuwa mimi ni
mtu wa Morogoro mwenzake, kwa hiyo nimuache Chameleone.
“Nilikubali walichokisema lakini kuanzia hapo, Chameleone na Merey
hawakupatikana. Merey alikuwa ‘bize’ na mambo yake, wakati Chameleone
hakutaka kupokea simu yangu kabisa.
“Siku moja nilibadilisha namba ya simu nikampigia Chameleone,
akapokea vizuri. Nikamkumbusha kuhusu fedha zangu, akaniambia hana uwezo
wa kulipa ila anachoweza kufanya ni mimi kuandaa shoo nyingine halafu
yeye atakuja ku-perform.
“Pamoja na kuahidi, kila nilipoandaa shoo, ukifika muda wake wa kuja
hakufanya hivyo. Hii inamaanisha kuwa Chameleone ana tabia ya utapeli na
Watanzania tunapaswa kuwa wamoja kwenye hili tatizo.”
JD alisema, ameamua kutokeza na kueleza haya kipindi hiki ili kila
mtu atambue kwamba Chameleone siyo mtu mzuri kwenye fedha na anaweza
kumkana promota wakati wowote.
No comments:
Post a Comment