Mtuhumiwa wa kwanza kwenye ishu ya kutekwa na kuteswa kwa mwenyekiti
wa Jumuiya ya Madaktari Dr Ulimboka Steven amekamatwa na jeshi la Polisi
baada ya kujisalimisha kwenye kanisa la ufufuo na uzima la Mchungaji
Jospephati Gwajima kwa lengo la kuungama dhambi zake.
Baada ya mtuhumiwa huyo ambae ni raia wa Kenya aitwae JOSHWA GITU
MUHINDI kwa mujibu wa hati yake ya kusafiria kukamatwa, amekiri kuhusika
kumteka na kumtesa Dr Ulimboka akiwa na wenzake 12 waliokodiwa na mtu
anaehisi kuwa anatoka serikalini.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amesema
walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusu kuwepo kwa mtu huyo
ambae imefahamika ni mwanachama wa kundi la GANGSTAR lenye makazi yake
Kenya na linaongozwa na Mtu anaetajwa kwa jina la SILENCER na sasa
wanaendelea na uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment