Tanzania ilimfahamu msanii
anaitwa Tanzanite baada ya kuanza kuimba juu ya beat za nyimbo za
Diamond Platnums kwa kutumia melody ile ile kasoro mashairi tu, kitu
ambacho pia alikua akikifanya bila ruhusa ya Diamond na kilishawahi
kuleta ugomvi kati yao.
Baada ya kukaa kwa muda, Tanzanite ametangaza msimamo wake wa sasa kwenye maisha ya sanaa.
Amesema “sasa hivi sikopi tena
nyimbo za wasanii wengine, kuna ngoma nimefanya na Kitale inaitwa
Namwaga radhi na hapa nipo kwenye mazoezi niko na dancers wangu kwa
ajili ya kufanya kitu cha ajabu, mwezi wa Ramadhani ukiisha watu
watarajie”
Tanzanite ambae ana kesi ya
ubakaji iliyomfanya awekwe segerea kwa miezi miwili kabla ya kupata
dhamana, amesema “sitamani sana kukopi natamani kuonyesha uwezo wangu
japo kuonyesha uwezo wangu mi mwenyewe imekua ngumu alafu nimeona kama
kukopi imekua njia rahisi sana kufanya vizuri, mi naona kukopi ndio
ilikua inanitoa sana kwa sababu nikifanya kitu changu nafasi sipati”
No comments:
Post a Comment