Aliyekuwa Rais wa shirikisho
linalotawala mchezo wa soka duniani, FIFA , Joao Havelange pamoja na
kiongozi wa soka wakati mmoja nchini Brazil Ricardo Teixeira
wanatuhumiwa kupokea mirungura ya mamilioni ya dola za kimarekani kama
hongo katika kupanga mwenyeji wa Kombe la Dunia, kwa mujibu wa tangazo
la FIFA lililochapishwa jumatano.
Hatimaye shirikisho hilo limechapisha hati ya
maelezo kamili kuwa Texeira alipokea faranga za Uswizi milioni 12.74
sawa na dola za Marekani milioni 13 kwa kiwango cha leo kuanzia mwaka
1992 hadi 1997 kama malipo kwa kampuni ya mauzo ya FIFA ikiwa ni
mshirika wa ISL. Kufilisika kwa kampuni hiyo yenye makao yake Uswizi
kulizusha upelelezi wa kihalifu na kufichua tabia mbovu iliyokuepo ya
viongozi kupokea mirungura ili kufanikisha mipango ya wanaohitaji.
Hati
hio yenye kurasa 41 ilionyesha kuwa Havelange alipokea malipo ya
faranga za Uswizi milioni 1.5 sawa na $milioni moja mnamo mwaka 1997,
mwaka mmoja kabla ya kumpisha Sepp Blatter kama Rais mpya.
Malipo yanayotajwa kuwa yalipitia benki za raia
hao wawili wa Brazil zilifikia kiwango cha faranga milioni 22 za Uswizi
kati ya mwaka 1992 na 2000.
Kiwango cha mirungura inayohusiana na hati
miliki ya kutangaza Kombe la Dunia pamoja na haki ya kupitisha matangazo
wakati wa Kombe la Dunia ilidhihirishwa katika taarifa iliyotayarishwa
na mwanasheria wa Wilaya ya Uswizi ya Zug aliyewachunguza Havelange na
Texeira kwa matumizi mabaya ya fedha au uongozi usioambatana na misingi
ya kazi.
Waraka huu mwanzoni uliwekewa kizuizi
usichapishwe tangu Juni mwaka 2010, baada ya wanasheria, FIFA na watu
wawili mashuhuri katika Soka duniani kuafikiana juu ya kusimamisha
upelelezi wa kihalifu.
FIFA, Havelange na Teixeira walirejesha faranga
milioni 5.5 million za Uswizi (takriban dola $6.1 wakati huo) ili
mwanasheria Thomas Hildbrand asimamishe uchunguzi na majina yao yawe ni
siri.
Teixeira, ambaye alirejesha faranga milioni 2.5,
alikanusha madai ya kuhusika kihalifu. Havelange, aliyerudisha laki
tano za Uswizi, hakutoa tamko lolote kuhusiana na madai ya uhalifu, kwa
mujibu wa taarifa hio.
No comments:
Post a Comment