GlaxoSmithKline kulipa faini ya $3b
Mojawapo wa kampuni kubwa zaidi
duniani ya dawa, GlaxoSmithKline, imekubali kulipa faini ya $3b katika
sakata ambayo imetajwa kuwa ulaghai mkubwa zaidi kuwahi kukumba sekta ya
afya katika historia ya Marekani.
Kampuni hiyo ya GlaxoSmithKline, inashutumiwa kuvunja sheria za Marekani kuhusiana na jinsi ilivyouza bidhaa zake mbali mbali.
Miongoni
mwa madai yanayokabili kampuni ya GSK ni kuwa kampuni hiyo ilijaribu
kuwashawishi wagonjwa walio chini ya umri wa miaka 18 kutumia madawa ya
dawa ya kupunguza simanzi, Paxil, ambaylo ilikuwa imeidhinishwa kwa watu
wazima wanaozidi umri huo pekee.
Naibu wa Mwanasheria Mkuu nchini Marekani, James
Cole aliwambia waandishi wa habari mjini Washington kuwa kesi hiyo ni
ya aina ya kipekee. Amesema malipo hayo ndiyo makubwa zaidi kuwahi
kutolewa kama faini katika historia ya huduma za afya katika historia ya
Marekani'.
Naibu huyo wa mwanasheria mkuu huyo alisema kuwa
kuna ushahidi kwamba kampuni hiyo ilijaribu kuwanunulia madaktari
vyakula na anasa zingine, ambazo zinaweza kutambuliwa kama hongo ili
watumie madawa ambayo hayakuwa yameidhinishwa.
Kampuni hiyo pia ililaumiwa kwa kutanganza matumizi ya dawa nyingine, Wellbutrin, kwa matumizi ambayo hayakuwa yameidhinishwa.
Kampuni hiyo imetoa taarifa na kusema kuwa haitarudia kosa hilo kwani imejifunza kutokana na makosa ya sasa.
No comments:
Post a Comment