Fifa kupigia kura 'Goal line technology'
Shirikisho la mchezo wa soka
duniani FiFa linajiandaa kupiga kura kuidhinisha matumizi ya
teknolojia-maarufu kama Goal Line technology- itakayo tumika kuamua
ikiwa mpira umevuka mstari wa goli au la.
Kumekuwa na shinikizo chungu nzima kwa
shirikisho la FIFA kufuatia makosa kadhaa yanayohusiana na maamuzi ya
mechi, ikiwemo kosa la hivi karibuni kuhusu mechi moja wakati wa
michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani ulaya.
Goli lililofungwa na Ukraine dhidi ya Uingereza
ilifutiliwa mbali licha ya picha za runinga kuonyesha kuwa mpira ulikuwa
umevuka na kupita mstari wa goli.
Shirikisho la FIFA linatarajiwa kuidhinisha
mifumo miwili, moja inayotumia kamera za video na nyingine inayotumia
sensa maalum ili kubainisha ikiwa mpira Umevuka mstari wa Goli.
No comments:
Post a Comment