CHUZ,ROSE WA CHUZ WAMWAGANA
Rose Michael ‘Rose wa Chuz’.
Tuesday Kihangala ‘Chuz’.
HATIMAYE ule uchumba wenye makeke wa Mkurugenzi wa Chuz
Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ na msanii wa kundi hilo, Rose
Michael ‘Rose wa Chuz’ umekatika na wawili hao wamemwagana, Risasi
Mchanganyiko lina ushahidi mkononi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wawili hao wamemwagana kufuatia timbwili
zito aliloliangusha Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ nyumbani kwa Chuz hivi
karibuni akimtuhumu demu huyo kumtesa mwanaye wakati baba mtu alipokuwa
Zanzibar ‘Zenji’ akirekodi filamu ya Dirty Game.
Habari zinasema baada ya Chuz kurejea kutoka Zenji, Rose alitoa
dukuduku lake kwamba, hawezi kuendelea kulea ‘toto ambalo’ mama yake
hana shukurani.
“Kisa cha hawa watu kumwangana ni Jini Kabula, Chuz alikwenda Zenji
kushuti filamu, aliporudi akakuta Rose amevimba macho kwa kulia,
alipoulizwa kasema Jini Kabula alimfanyai fujo akimtuhumu kumtessa
mwanaye.
“Chuz alijaribu kumlainisha Rose kwa maneno ‘matamtam’ lakini
hakukubali, akaondoka kurudi kwao Arusha, hivi leo (juzi, Jumatatu)
ninavyoongea na wewe, Rose yupo Arusha kwa wazazi wake,” kilisema chanzo
hicho.
Paparazi wetu alimsaka Chuz kwa simu ya kiganjani na alipopatikana na kusomewa mashitaka yake, alikuwa na haya ya kusema:
Chuz: Aaah! Kifupi ni kwamba, ‘asa hivi mi naangalia kazi bwana.
Unajua filamu za Bongo zinauza sana, lakini hata hivyo, tumejitahidi
kuwa kama Wanaijeria, si eti?”
Risasi Mchanganyiko: Jibu swali langu, ni kweli umemwagana na Rose?
Chuz: Rose yupo, unajua yule demu (Rose) atakuja kuwa staa mkubwa
sana haba Bongo, mi nakwambia. Anajua kuuvaa uhusika katika filamu. Ha!
Ha! Ha! Ha!
Rose alipopigiwa simu siku ya Jumatatu iliyopita hakuweza kupatikana mara moja hewani.
Mapema mwaka huu, moja ya magazeti ya Global Publishers liliripoti
Chuz kutangaza hadharani kwamba Rose ni mchumba wake na wangefunga ndoa
katikati ya mwaka huu. Aliongeza kuwa msichana huyo ndiye mwanamke wa
maisha yake baada ya wote waliopita.
Hata hivyo, Gazeti la Amani likaja andika habari zilizotoka kinywani
mwa Jina Kabula akimuasa Rose kuwa makini na Chuz kwamba katika wanaume
waongo ulimwenguni, jamaa huyo anashika nafasi ya pili.
Mbali na Rose, Chuz ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasanii wa filamu, Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’, Joan Mutovolwa, Leila Ismail ‘Lilly’ (amezaa naye) Miriam Jolwa Jini Kabula (amezaa naye).
Mbali na Rose, Chuz ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasanii wa filamu, Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’, Joan Mutovolwa, Leila Ismail ‘Lilly’ (amezaa naye) Miriam Jolwa Jini Kabula (amezaa naye).
No comments:
Post a Comment