Usain Bolt amesema amejiandaa
kikamilifu kuutetea ubingwa wake wa mashindano ya Olimpiki katika mbio
fupi, licha ya kwamba kwa hivi sasa anasema yeye ni mzima asilimia 95.
Bolt, bingwa wa mbio za mita 100 na 200, anasema
kwa kiasi fulani ameweza kupata nafuu baada ya kupambana na matatizo ya
mgongo na misuli, na anahisi ataweza kuutetea ubingwa wake katika mbio
hizo fupi.
Mwanariadha huyo wa Jamaica, akizungumza na
mwandishi wa michezo wa BBC, David Bond, amesema licha ya kwamba yeye si
mzima kwa asilimia 100, ataweza kuhifadhi ubingwa huo, na kuandikisha
historia mjini London.
Bolt alitamka hayo ikiwa sasa ni miaka minne
tangu alipovunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 100 katika mashindano
ya Beijing ya mwaka 2008, kwa kuandikisha muda wa sekunde 9.69, licha ya
kupunguza kasi na kuanza kufanya sherehe hata kabla ya kuvuka msitari
wa kukamilisha mbio.
No comments:
Post a Comment