Kwa mara ya kwanza Big brother
wameandika kwenye website yao kwamba jumapili usiku July 15 2012 wakati
wa Eviction ndio wameona mshiriki akilia na kuhusunika kiukweli, sio
kwamba washiriki walioondoka walikua na furaha bali walijaribu kuficha
huzuni zao kwa plastic smiles
Goldie alikosa cha kuongea na
kufanya hata maneno yake ya mwisho kwenye interview yasisikike kutokana
na huzuni aliyokua nayo, maumivu makubwa aliyapata baada ya kuoyeshwa
video ambayo mshkaji wake ambae ni Keitta akimpigia kura atoke kwa
sababu anaona Goldie anafake life.
Hicho kitu kilimfanya Goldie
kulia kiukweli kwa sababu alikua mshkaji wa Keitta na Keitta hakuwahi
kuonyesha ishara yoyote kwamba angemgeuka kiasi hicho, alisema “nimekua
karibu na Keita, nimekua nikimpikia alafu kanipigia kura nitoke?
No comments:
Post a Comment